Masaa kadhaa baada ya Carlo Ancelotti kupoteza ajira yake katika klabu
bingwa ya Ujerumani – FC Bayern Munich kutokana mfululizo wa matokeo
yasiyoridhisha – Rais wa klabu hiyo Uli Hoeness ametaja moja ya sababu
kuu zilizosababisha uongozi wa Bayern kuamua kuivunja ndoa yao na
Ancelotti.
Uli Hoeness anasema kulikuwa na wachezaji wakubwa watano ambao walishakuwa hawana imani na kocha na walianza kumpinga.
“Kulikuwa na wachezaji watano ambao walikuwa wanampinga na hilo likawa
jamho gumu kwenye utendaji wa kazi,” aliiambia Funke Sport.
“Kama kocha huwezi kuwa na wachezaji wakubwa kwenye kikosi chako ambao
wanakupinga. Nimejifunza hili maisha yangu yote na msemo usemao; Adui
aliyepo kitandani kwako ndio hatari zaidi.’ Kutokana na jambo hilo
ilitubidi kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Mr. Ancelotti.”
Carlo Ancelotti akiwa na Bayern Munich ana rekodi ya kuiongoza katika
mechi 60, wameshinda 42, sare 9 na wamepoteza mechi 9. Timu yake
ilifunga magoli 156, na pia waliruhusu magoli 50 kutinga kwenye nyavu
zao. Ameshinda Bundesliga mara moja na DFL Supercup mara 2.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, PSG, Real Madrid na AC Milan ameshinda
ubingwa wa ulaya mara 3 akiwa na Milan mwaka 2003 na 2007, akashinda La
Decimal na Madrid mwaka 2014.
Idadi hii inamfanya kuwa mmoja kati ya makocha wawili waliofanikiwa
zaidi katika historia ya michuano ya ulaya sambamba na kocha wa zamani
wa Liverpool Bob Paisley, ambaye alishinda ubingwa wa ulaya miaka ya
1977, 1978 na 1981.
No comments:
Post a Comment