Ajali ilivyotokea.
Mtalii wa Ufaransa amepongezwa baada ya kunusru vifo vya watu zaidi ya 21 waliotaka kufa ajalini nchini Australia.
Mtalii huyo alikuchukua hatua za haraka kulizuia basi lililokuwa likielekea kupinduka mtaroni Milima ya Alps nchini Austria baada dereva wa abasi hilo kuzirai ghafla wakati likiwa kwenye mwendokasi.
Basi hilo lilikuwa likipita katika eneo la milima hiyo, raia huyo wa Ufaransa aliliona likiseleleka mtaroni na kuelekea kupinduka ndipo akachukua jitihada za haraka kunusuru maisha ya watu hao kwa kuweka gogo refu ambapo basi hilo liligonga na kukwama.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa hospitali kutibiwa huku dereva wake mwenye umri wa miaka 76 akiwa bado amezirai na chanzo cha kurizai kwake hakikujulikana.
Abiria mmjoa raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 aliyekuwa ameketi karibu na kiti cha dereva, alichomoka na kiti chake wakati gari hilo lilikuwa linagonga gogo hilo na kukimbizwa katika Hspitali ya Schwaz Magharibi mwa Austria.
Mwaka 2004, watalii watano waliuawa wakati basi liliacha barabara na kupingira chini ya mlima karibu ni Kijiji cha Bad Dürrnberg nchini humo.
No comments:
Post a Comment