Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe leo Septemba 22, 2017 amezungumza na vyombo vya Habari Jijini Dar es salaam kuhusu hali ya Tundu Lissu na mengine yanayoendelea nchini kwasasa.
Hizi ni baadhi ya sentensi zilizonukuliwa kutoka kwenye hotuba yake ya leo.
"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Tundu Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii"- Mbowe
"Ni nani katika vyombo vya ulinzi na usalama, simjui lakini ni vigumu sana kusema tukio la ujambazi, hakuna ujambazi pale." Mbowe.
"Kama serikali inajiamini iko safi kabisa, waruhusu wachunguzi huru kama Scotland Yard waje wafanye uchunguzi kwani hatuna imani na Polisi"- Mbowe
"Mashine yetu Tundu Lissu itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%"-Mbowe
"Waziri Ummy Mwalimu anasema kwamba, serikali ipo tayari kumtibu Tundu Lissu mahala popote dunia, hapo unajiuliza, kwani Kenya si duniani?"- Mbowe
Freeman Mbowe: Spika amesema nimtumie barua, ili aseme kwamba nimemuomba wakati yeye alikuwepo hospitali, ajiandikie mwenyewe.
"Jaji Mkuu anasema uchunguzi utafanyika ndani, tunamwambia asubiri ushahidi Mahakamani, uchunguzi ni mambo ya Polisi"- Mbowe
Freeman Mbowe: Wabunge kutibiwa na serikali ni haki stahiki, Lissu amepata matatizo akiwa kazini.
"Hadi leo bado hatujapokea michango iliyochangwa na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"- Mbowe
Freeman Mbowe: Nawashukuru sana wanahabari mmeripoti tukio hili usiku kucha. Naomba muwe makini na habari pia zinazotolewa.
No comments:
Post a Comment