Burundi hali si Shwari;Amnesty International
Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty
International limeonya kuwa Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaorudi
nchini kwao kutoka Tanzania wanakabiliwa na hatari za kiusalama nchini
mwao. Mwezi uliopita, Tanzania, Burundi na shirika la umoja wa mataifa
linalohudumia wakimbizi UNHCR walikubaliana kwamba kufikia mwisho wa
mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi elfu kumi na mbili wanaoishi
Tanzania na wanataka kurudi kwao Burundi kwa hiari.
Lakini Amnesty International inasema, mpango huu unahatarisha maisha ya
maelfu ya wakimbizi na linaamini kuwa wakimbizi wengi wanarejeshwa
nyumbani kwao kutokana msukumo wa ushawishi kutoka serikali ya Tanzania
na Burundi.
Shirika hilo limedai kuwa hali ya usalama bado sio shwari katika ripoti
yao inayotoka leo,wanasema visa vya kuteswa,kufungwa bila makosa
,kubakwa na hata kuuwawa bado vinaendelea.
No comments:
Post a Comment