Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia
Ackson (wa tatu kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki Kiongozi wa Kundi
la Ngoma la Kannengwa Rungwe, Nolbert Mwandinga, baada ya kundi lake
kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Ingoma Kituli, wakati wa hafla
ya kutoa zawadi kwa washindi wa Tamasha la Tulia Traditional Dances
Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale
Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya
washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia
Ackson akicheza ngoma ya asili ya kundi la Banyampulo ya kabila la
Wanyakyusa, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances
Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale
Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla ya
washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
Wacheza Bao Gabriel Mwasankinga wa timu
ya CCM (kushoto) akichuana na Pascal Mbwelembweta wa timu ya Kawechele,
kutafuta mshindi wa tatu katika mchezo wa fainali za mchezo huo
kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2017,
lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu Wilaya
ya Rungwe mkoani Mbeya.
Wacheza Bao Kocha Lufingo wa timu ya
Stendi Kuu (kushoto) akichuana na Six Willson wa timu ya Soko Kuu,
kutafuta mshindi wa kwanza na wapili katika mchezo wa fainali za mchezo
huo kuadhimisha Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival
2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Tandale Tukuyu
Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia
Ackson, akipokea michango ya hela kutoka kwa wananchi wa Tukuyu kwa
ajili ya harambee ya kuichangia timu ya Tukuyu Stars ”Changia Tukuyu
Stars irudi Ligi Kuu” wakati wa Tamasha la Tulia Traditional
Dances Festival 2017, lililomalizika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa
Tandale Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika Tamasha hilo jumla
ya washindi 10 wa kwanza kutoka kila kundi walizawadiwa Pikipiki.
Picha na Muhidin Sufiani
No comments:
Post a Comment