Sunday, 24 September 2017

Tuzo ya ushairi ya Ebrahim Hussein

Washindi 3 wa tuzo ya ushairi ya Ebrahim Hussein wakiongozwa na Mwanamke ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha SAUTI Jijini Mwanza Nusura Msafiri Haji wametangazwa jana jioni Septemba 23 sambamba na kukabidhiwa vyeti na pesa taslimu ambapo mshindi wa kwanza alipewa cheti na Tsh milioni 2, akifuatiwa na mshindi wa pili Erick Ndumbaro aliyepewa milioni 1 na nusu na watatu Hamisi Kisamuu akipewa molioni 1.


 Hafla ilifanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kukabidhi tuzo hizo mgeni rasmi Balozi wa Swaziland Arthur Mattii katika nchi za Afrika Mashariki amepongeza jitahada za kukuza lugha ya Kiswahili.

Waandaaji wameeleza kuwa hii ni mara ya tatu kwa tuzo hiyo kutolewa. Taarifa hiyo inabainisha kuwa tuzo hiyo ilibuniwa kama njia ya kuendeleza na kukuza ushairi na lugha ya Kiswahili.

Shindano hili la tatu lilianza rasmi Novemba 4, mwaka jana na kukamilika April 30, ambapo jopo la majaji, likiongozwa na Profesa Mugyabuso Mlinzi Mulokozi wa UDSM, ameeleza kuwa lilipitia kazi zote zilizowasilishwa, na kwamba mashairi hayo yalilenga zaidi kwenye matatizo ya Watanzania
.


Kamati ya Usimamizi ya Tunzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Demere Kitunga, imeendesha shindano hili kwa kushurikiana na Tanzania Gatsby Trust (TGT) na Mkuki na Nyota Publishers.
Washairi wengi walitokea Dsm, Mbeya, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza na katika baadhi ya mikoa mingine
Tuzo hiyo imeanzishwa kutokana na matakwa ya mtengeneza filamu raia wa Canada, marehemu Gerald Belkin, ambaye pia alitaka iitwe kwa jina la rafiki yake, mshairi maarufu na muandaaji wa filamu, Profesa Ebrahim Hussein.


No comments:

Post a Comment