Abner Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura alisema kuwqa hakuna mtu anayetumia umeme aliye na huduma hiyo kwa sasa.
Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema kuwa mafuriko makubwa yanaikumba nchi hyo, Maria kwa sasa kinaondoka nchini Puerto Rico na kumepunguza nguvu zake hadi kiwango cha pili.
Hi ni hatua ya kuwazuia watu kupata ajali kutokana na nyaya za umeme zilizoanguka na vifuzi vilivyo barabara za mji.
Mapema Bw Rossello alimuomba Rais Donald Trumo kukitangaza kisiwa hicho kuwa eneo la janga baada ya kimbunga kusababisha mafuriko makubwa na upepo unaotishia maisha.
Kimbunga hicho tayari kimesababisha vifo vya watu 7 katika kisiwa cha Dominica ambacho kiliathiriwa vibaya siku ya Jumatatu.
No comments:
Post a Comment