Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern
Lumbanga (kushoto) akiongea wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof.
Sufian Bukurura.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka
ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga
wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern
Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na wajumbe wengine wa Bodi(hawapo
pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern
Lumbanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo ameahidi
kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka taratibu za manunuzi
zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017.
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt. Laurent Shirima akiongea,
wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti
ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali imesema itazichukulia
hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni za manunuzi ya Umma
pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo zimebainika katika
ripoti ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma
na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akipokea
ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za Serikali katika sekta ya
Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
“Tutazichukulia hatua na
kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti hii kuwa na
viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika manunuzi
yao,” alisema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa, zaidi ya
70% ya fedha za Umma zinatumika kununua vifaa na huduma mbalimbali
hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo zinatumika bila kufuata
sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga amezitaja taasisi ambazo
zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa mwaka 2016/2017 kuwa ni
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taasisi nyingine ni Shirika la
Bima la Taifa (NIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya
Anga (TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na Halmashauri ya Wilaya
Kondoa.
Balozi Lumbanga amesema kuwa
uchunguzi wa zabuni mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 160.5 ambazo
zilikuwa zinatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja TCAA
haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA ilipendekeza utekelezaji wa
miradi hiyo uendelee kama ilivyopangwa.
“Uchunguzi uliofanywa katika
taasisi sita zilizobaki ulibaini kuwa Serikali ilipata hasara ya
takribani shilingi milioni 12.15 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo,
ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi uliosababisha ongezeko la riba
pamoja na faini zilizotokana na ukiukwaji wa taratibu za kijamii na
mazingira kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa kazi za ujenzi,” alisema
Balozi Lumbanga.
Balozi Lumbanga amezitaja Taasisi
zilizobainika na malipo yenye utata kuwa ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya Kwimba.
Ukaguzi wa kupima upatikanaji wa thamani ya fedha ulibaini malipo yenye
utata katika taasisi hizo tatu ambazo ni kiasi cha shilingi milioni
483.44 zililipwa kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.
Vile vile amesema kuwa, miradi 33
katika taasisi 17 ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya
rushwa. Taasisi hizo ni Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka za Moshi
(Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na Arusha (Auwasa) pamoja na Halmashauri ya
Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo na Moshi.
Taasisi byingine ni Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara ya Maji na Umwagiliaji,
Chuo cha Ufundi Arusha, Halmashauri ya Mjia wa Kahama, Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Ofisi ya Katibu
Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Mji wa MAsasi pamoja na Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti ya 11 kuwasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa.
No comments:
Post a Comment