Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
ufunguzi mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya
ya Madola ambao alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Majaji na Mahakimu wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Madola wakimsikiliza Makamu wa Rais Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua
mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John
Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa
Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, Makamu wa
Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Chama cha Majaji na
Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola (CMJA). Makamu wa Rais
alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango na uhuru
wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria vimeendelea
kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”.
Kwa miaka mingi mmeendelea
kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku mkijitahidi kuendeleza
utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya madola, alisema Makamu wa
Rais.
Aidha, mkutano huo
uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na mahakimu, Makamu wa
Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono jitihada za serikali
katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili kufikia maendeleo ya
kweli. “Naamini kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi,
uwajibikaji na jumuishi haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga
na jitihada za serikali za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza
Makamu wa Rais.
Pia Makamu wa Rais alisisitiza
kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na hivyo kupoteza utawala wa
sheria. Aliwataka washiriki wa mkutano huo kupambana na rushwa katika
mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo vinapatikana.
Mwisho Makamu wa Rais
aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali ya Tanzania
itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa kuhakikisha
inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa.
Imetolewa na :-
Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment