Monday, 25 September 2017

Silaha kutoka Uturuki Zanaswa Nigeria

kikosi cha jeshi la nchini Nigeria
Serikali ya Nigeria imekamata silaha zilizokuwa zinaingizwa nchini humo kupitia bandari ya Lagos kinyume cha sheria, kutoka nchini Uturuki.
Ni mara ya nne sasa tukio kama hilo linajiri katika nchi hiyo yenye kukumbwa na makabiliano ya mara kwa mara ya Boko Haram. Balozi wa Uturuki jijini Lagos ametakiwa kujieleza katika mamlaka ya mipaka.
Jumla ya silaha elfu tatu zinadaiwa kukamatwa katika bandari ya Lagos na idara ya forodha tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Viongozi wa idara ya forodha nchini Uturuki wanawatuhumu kundi la wafanyabiashara haram ya silaha kutoka nchini Nigeria ambao wanafanya biashara hiyo kutoka Uturuki.
Hata hivyo viuongozi wa nigeria wanajaribu kufanya uchunguzi kufahamu wapi zinapoelekea silaha hizo.
Hapo awali Uturuki ilijieleza kwamba haihusiki kwa vyovyote vile na biashara hiyo, na kwamba taarifa hizo ni kutaka kuichafua.

Mwezi Mei silaha 440 zilikamatwa na meli ambayo ilielezwa kwamba ilikuwa ikitokea nchini Marekani ambapo ilifanya kituo nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment