Merkel ashinda uchaguzi mkuu
Kansela wa ujerumani , Angela Merkel ameibuka kuwa mshindi katika
uchaguzi mkuu nchini humo kwa kipindi cha nne. Hata hivyo mamlaka yake
imepungua kutokana na uungwaji mkono mdogo ndani ya chama chake chenye
mrengo wa kati kutokana na kuimarika kwa chama cha kulia yaani AFD.
Inakadiriwa kuwa chama chenye msimamo mkali dhidi ya wahamiaji cha AFD
kinakadiriwa kuwa kwa mara ya kwanza kitashinda asilimia 13 ya viti
bungeni.
Mwenyekiti wa chama cha AfD Frauke Petry, anasema Wajerumani wameshuhudia tetemeko la ardhi kisiasa nchini humo.
Aidha Merkel ameonyesha kutofurahishwa na matokeo ya chama chake. Hata
hivyo haya ni matokeo mengine mabaya kuwahi kutokea katika chama chake
katika historia ya Ujerumani, tangu yale ya 1933 yaliyo muweka
madarakani Adolf Hitler.
No comments:
Post a Comment