Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Raya Issa Msellem akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu
mkutano wa saba wa Baraza la tisa la Wawakilishi huko Chukwani Zanzibar.
Mshauri wa Baraza la Wawakilishi
mambo ya sheria Mussa Kombo Bakari akitowa ufafanuzi juu ya maswali
yaliyoulizwa na baadhi ya Waandishi wa habari huko Chukwani nje kidogo
ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar.
Na Khadija Khamis –Maelezo
Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Raya Issa Mselem amesema Mkutano wa saba wa Baraza la
Wawakilishi unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano tarehe 27 Septemba mwaka
huu .
Aliyasema huko katika Ukumbi wa
Baraza la Wawaklishi Chukwani nje kidogo ya Zanzibar wakati akizungumza
na waandishi kutoka katika vyombo mbali mbali vya habari
Alisema shughuli ambazo
zinatarajiwa kufanyika katika mkutano huo ni maswali 136 ambayo
yanatarajiwa kujibiwa katika kikao hicho pamoja na miswaada miwili
itawasilishwa kwa mara ya pili katika kikao hicho.
Aidha alisema mswada
itayowasilishwa ni mswada wa sheria yakufuta sheria ya mahakama ya
kadhi namba 3 ya 1985 na kuanzishwa upya mahakama ya kadhi na kuweka
masharti menghine yanayohusiana na hayo na mswada mengine ni mswada wa
sheria yakuanzishwa baraza la taifa la biashara na kuweka mambo mengine
yanayohusiana na hayo.
Alieleza kuwa katika mkutano huo
pia utapokea ripoti za utekelezaji wa Wizara za SMZ kuhusu maagizo
ya kamati za kudumu za baraza pamoja taarifa za seriikali na ripoti za
utekelezaji wa mamlaka ya maji Zanzibar(ZAWA).
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment