Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika
uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo jinsi ya kutoa huduma ya afya kwa
watoto wachanga wenye umri sufuri hadi siku 28. Uzinduzi huo umefanyika
leo katika hospitali hiyo.
Madaktari na wauguzi wakiwa kwenye
mkutano wa kuzindua kitabu kinachoelezea jinsi ya kuwahudumia watoto
wachanga baada ya kuzaliwa.
Daktari wa watoto wa hospitali hiyo, Dk. Judith Cosmas ambaye ameshiriki kuaanda kitabu hicho akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkuu wa Idara ya Watoto, Dk. Merry
Charles akisisitiza jambo huku akionyesha kitabu hicho ambacho kitakuwa
kikitumika wakati wa kuwahudumia watoto hao.
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru (kaunda suti) akiwa kwenye mkutano huo leo.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya MNH na wadau mbalimbali.
Dar
es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imezindua
muongozo utakaosaidia kuwahudumia watoto wachanga( Neonatal Guideline)
wenye umri kuanzia siku 0 hadi siku 28 ili kuhakikisha wanapata huduma
inayostahiki.
Muongozo
huo umeandaliwa na madaktari wa MNH na kupitiwa na wadau mbalimbali
wakiwemo wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) pamoja na Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal kilichopo
Afrika Kusini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru
amesema muongozo huo si tu unamanufaa kwa MNH bali pia una manufaa kwa
hospitali zingine kwani utawezesha mtoto kupata tiba inayotakiwa hata
sehemu ambazo hakuna watalaam.
Kwa
upande wake Daktari Bingwa wa Watoto Edna Majaliwa ambaye pia ni Mkuu
wa Kitengo cha Watoto Wachanga wa hospitali hiyo amesema kuwepo kwa
muongozo huo kutasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga sanjari na
kupunguza rufaa za watoto hao kuletwa Muhimbili .
‘’
Kusudio letu ni kuendelea kupunguza vifo vya watoto wachanga , MNH
tumefanikiwa kupunguza vifo hivyo kutoka 26 kwa kila vizazi hai 1,000
na kufikia 18 kwa kila vizazi hai 1,000. Kwa mwaka watoto wanaozaliwa
hapa ni takribani 10,000 hivyo naamini muongozo huuu utaleta
mabadiliko makubwa‘’ amesema Dk. Majaliwa.
Pia
ameelezea vyanzo vinavyosababisha vifo vya watoto wachanga kuwa ni
madhara ya kuwa njiti, mtoto ambaye amezaliwa na hakulia pamoja na mtoto
mwenye vimelea vya bakteria.
Akiwasilisha
mada kuhusu muongozo huo , Daktari wa watoto , Jullieth Cosmas
ametaja sababu zinazochangia watoto wachanga kulazwa Hospitalini kuwa
ni mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(Njiti) mtoto kushindwa kupumua
vizuri pindi anapozaliwa , mtoto kupata maambukizi , mtoto kutolia
wakapi alipozaliwa na mtoto kuumia wakati akizaliwa.
No comments:
Post a Comment