Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya
(kulia) akitembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo ili kuona
maeneo mbalimbali yaliokarabatiwa vikiwamo vyumba vya upasuaji na vyumba
vya kulaza wagonjwa wa figo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulusubisya
akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Uzingizi leo pamoja na watumishi
wengine wa hospitali hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa idara
hiyo pamoja na watumishi wengine mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akimkaribisha Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dk. Ulusubisya kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo
leo.
Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwamo wa Idara ya Usingizi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Muhimbili, Profesa Museru.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Dar es salaam
Serikali
imepongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) za
kuboresha huduma sanjari na kuwawezesha watalaam kusoma ili wapate
ujuzi zaidi na kutoa huduma bora na za kibingwa.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulusubisya wakati
akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo kupitia Idara ya Usingizi.
Dk.
Mpoki amesema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na uongozi wa
hospitali na kwamba hatua hiyo inaleta faraja kwa Watanzania kwani sasa
wana uhakika wa kupata huduma bora .
“Naona
mabadiliko makubwa hapa Muhimbili, mmeongeza vyumba vya upasuaji,
Vyumba vya wagonjwa mahutuni (ICU) na pia mnaendelea kuboresha huduma
zingine kwakweli hatua hii ni ya kupongezwa na ninaomba muendelee
kujituma kwani hospitali hii inategemewa kwa sababu mna watalaam wengi
waliobobea hapa,’’ amesema Dk. Mpoki.
Kuhusu
kusomesha wataalam, Katibu Mkuu amesema hatua hiyo ni nzuri kwani
watalaam hao watapata fursa ya kuwatawafundisha wengine ili nao wapate
ujuzi .
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa
Lawrence Museru amesema MNH inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo upungufu wa wataalam katika Idara ya Usingizi na kwamba
hospitali inaendelea kutatua changamoto hizo.
Dk.
Mpoki ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dk. Doroth
Gwajima pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kutembelea maeneo
mbalimbali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo vyumba vya upasuaji,
wodi ya wagonjwa mahututi na wodi ya watoto.
No comments:
Post a Comment