Mjumbe wa Sekretarieti toka
Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Saum Rashid akisisitiza jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa,
katikati ni Bi. Angelina Mutahiwa na kulia ni Bi. Dominata Rwechungura
wajumbe wa Sekretarieti hiyo.
Baadhi ya waandishi wa Habari
wakimsikiliza Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake
Bi. Angelina Mutahiwa (aliyekaa katikati) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa.
Mjumbe wa Sekretarieti toka
Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa,
kushoto ni Bi. Saum Rashid na kulia Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa
Sekretarieti hiyo.
Mjumbe wa Sekretarieti toka
Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Angelina Mutahiwa akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu
udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa,
kushoto ni Bi. Saum Rashid na kulia Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa
Sekretarieti hiyo.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo
Na Thobias Robert- MAELEZO
29-09-2017
Taasisi isiyo ya kiserikali
inayoundwa na Jumuiya za Wanawake wa Vyama vyote vya siasa (Ulingo)
imelaani vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii
vinavyofanywa na baadhi ya watu dhidi ya viongozi wanawake wana siasa
pamoja na serikali kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Saum Rashid alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kwaaajili ya kulaani watu wanaotumia
mitandao ya kijamii kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima viongozi
wanawake.
“Matusi ambayo wanatupiwa na watu
wasio na maadili ni matusi siyo kwa wahusika tu bali kwa wanawake wote,
hivyo ikumbukwe kuwa hao wanaowalenga wanafamilia, watoto na marafiki na
wanaongoza mamilioni ya watanzania,” alifafanua Bi. Saum.
Akizungumza bila kuwataja
wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kudhalilisha viongozi, Bi.Saum
alisema wanawake wanapodhalilishwa hasa na wanawake wenzao inawakatisha
tamaa katika kutimiza majukumu yao hivyo akaomba mamlaka husika
kusimamia Sheria ili mitandao isitumike vibaya.
Aidha Bi. Saum amesema kuwa
anaamini viongozi wanawake ambao wamepewa heshima na dhamana ya
kuongoza, wana uwezo mkubwa na wanastahili kuwa kwenye nafasi walizo
nazo .
Taasisi hiyo ambayo
inawashirikisha pia watu wenye ulemavu imelaani vikali vitendo vya
udhalilishaji na kuwataka watanzania warejee kwenye misingi ya utu na
kuthaminiana kama maadili ya kitanzania yanavyoelekeza hasa kwa watoto
wa kike.
Kwa upande wake Angelina Mutahiwa
ambaye pia ni Mjumbe wa taasisi ya Ulingo alisema kuwa, mwanamke ni
mlezi mzuri wa maadili katika jamii hivyo kumdhalilisha ni kuvunja
malezi na maadili katika jamii na kuchochea vitendo viovu dhidi yake
ambavyo vitadumu kizazi hadi kizazi.
“Wale wachache ambao wameonesha
utovu wa nidhamu kwa kuendelea kumnyanyasa mwanamke watambue kwamba wao
hawapo juu ya sheria na katiba ya nchi iko wazi hairuhusu mwanamke
kudhalilishwa, kuonewa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili haikubaliki
na hatutakubali,” alisistiza Bi.Mutahiwa.
Ulingo ni taasisi isiyo ya
kiserikali inayoundwa na jumuiya za wanawake wa vyama vyote vya siasa
vilivyosajiliwa kwenye na Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kwa
lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika nyanja mmbalimbali ili waingie
kwenye vyombo vya maamuzi.
Taasisi hiyo kwa sasa inapigania
haki sawa kwa wanawake yaani 50/50 kwani waaamini kuwa uongozi ni haki
ya kila mtu kwa maana ya wanawake na wanaume.
No comments:
Post a Comment