Friday, 22 September 2017

Wanasayansi watengeneza kinga inayoweza kushambulia HIV kwa 99%

Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.
Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.
Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiani baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni maduka ya dawa ya Sanofi.
Shirika la kimataifa la kukabiliana na ukimwi -International Aids Society linasema kuwa huu ni "ugunduzi wa kihistoria ".
Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV
Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake.
Aina kadhaa za virusi vya HIV - katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi.
Kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili najipata katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Lakini baada ya miaka kadhaa ya maambukizi, wagonjwa wachache hujenga silaha kali ya mwili ambapo " Mwili hupunguza uharibifu wa kinga ya mwili " kwa kushambulia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya HIV.

Watafiti wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuwia maambukizi hayo mapema.

No comments:

Post a Comment