Kuna rekodi moja ya Bundesliga inayoziunganisha Borussia zote yaani Monchengladbach na Dortmund.
Wakiwa wanajiandaa kukutana katika
dimba la Signal Iduna Park katika mechi kali ya wiki hii Siku ya
jumamosi, kitu cha uhakika ni kwamba rekodi hiyo haitavunjwa.
Kwenye mechi ya mwisho wa msimu wa
1977/8, Monchengladbach waliingia uwanjani wakiwa na idadi sawa ya
point na Cologne, lakini wakiwa nyuma kwa tofauti ya magoli 10 nyuma ya
wapinzani wao ambao walikuwa wanatazamia kushinda kirahisi mchezo wao
dhidi ya St Pauli.
Kwenye mchezo uliolalia upande
mmoja zaidi katika historia ya Bundesliga, Monchengladbach walifunga
mabao sita katika kila dakika 45 za mchezo bila majibu hivyo kupelekea
matokeo ya 12-0 baada ya kipenga cha mwisho kulia. Ikiwa ni rekodi
ambayo haijavunjwa hadi sasa ndani ya Bundesliga.
Tangu kipindi hicho
Monchengladbach hawajakaribia hata kidogo kushinda ubingwa wao wa sita
huku wapinzani wao wakishinda Ubingwa huo mara tano na kuwa ndio hasimu
mkubwa wa Bayern Munich.
Japokuwa idadi ya zaidi ya watu
80,000 hawatarajii kuona rekodi ya mabao 12 ikivunjwa, wanaweza
kutazamia mchezo ambao bado utakuwa na mabao mengi ukizingatia timu hizi
zina uwezo mzuri wa kushambulia na soka la kuvutia. Michezo 5 ya nyuma
waliyokutana umeshuhudia angalau idadi ya magoli manne kwenye kila
mchezo.
Mfungaji bora wa msimu uliopita
Pierre Emerick Aubameyang ameendelea kutikisa nyavu bila wasi, huku
Monchengladbach wakiwa na vijana machachari Lars Stindl na Thorgan
Hazard, ambao wanachezea timu za taifa, Ujerumani na Ubelgiji.
Mchezo huu pia utakuwa ni kwanza
kwa kiungo Mahmoud Dahoud kukutana na timu yake ya zamani tangu
alipojiunga na Dortmund majira ya joto. Nafasi yake katika kikosi cha
Monchengladbach imejazwa na kinda kutoka Uswizi Denis Zakaria ambaye
amepata sifa kedekede kutoka kwa kocha wake.
“Ni burudani unapomtazama Denis
namna alivyozoea. Hakika ameshatulia ndani ya Bundesliga”, Kocha wa
Monchengladbach Dieter Hecking alisema, “Lakini sasa anahitaji kuendelea
kucheza vizuri bila kuonyeshwa kadi”, aliongeza.
Watazamaji kote nchini wataweza kutazama mchezo huu MUBASHARA kupitia Chaneli ya World Football Saa 1:30 Usiku Jumamosi hii.
Hii ni moja kati ya mechi
zinazofanya Bundesliga iwe na mvuto wa kipekee na pia nafasi kwa
waafrika kumtazama muafrika mwenzetu Aubameyang ambaye ni kinara ndani
ya timu ya Dortmund.
No comments:
Post a Comment