Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa
kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta
ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa na kulia ni Mjumbe
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold Mfungahema
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa
kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta
ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Mwakilishi kutoka kampuni ya IPSOS
inayokusanya takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji Bw. Samuel Muthoka
akiwasilisha taarifa ya namna kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa
kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta
ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka African Swahili
Televisheni akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na
usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa watatu kulia) katika
picha ya pamoja na wadau walioshiriki kikao cha wadau wa ukusanyaji na
usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es
Salaam. Watatu kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
Na. Neema Mathas- MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku matumizi ya
takwimu zinazotolewa na kampuni ya GeoPoll zinazohusu Kiwango cha
wananchi kusikiliza na kutazama vituo vya Redio na Televisheni hapa
nchini kwa kuwa takwimu hizo zina mapungufu makubwa.
Waziri Mwakyembe alitoa agizo hilo
jana jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na makampuni ya ukusanyaji
na usambazi wa takwimu kwa upande mmoja na watumiaji wa takwimu ambao ni
vituo vya Redio na Televisheni kwa upande mwingine.
Katika kikao hicho cha pamoja,
makampuni ya IPSOS Tanzania, Push Observer na GeoPoll walifafanya
mawasilisho ya namna wanavyokusanya takwimu wakati Ofisi ya Taifa ya
Takwimu yenyewe ilifanya wasilisho la kuonesha njia bora na sahihi za
ukusanyaji na usambazaji takwimu. Hata hivyo kamapuni ya Geopoll
haikuhudhuria kikao hicho.
“Nimeamua kuzuia utumiaji na
usambazaji wa takwimu za kampuni ya GeoPoll hapa nchini baada ya
kugundua tafiti za hii kampuni zina mapungufu makubwa na kusababisha
malalamiko mengi kutoka kwa wadau na wamiliki wa vituo mbalimbali vya
radio na televisheni,” alieleza Waziri.
Kutokana na kupigwa marufuku
matumizi ya takwimu za GeoPoll nchini, Waziri pia ameyataka makampuni
yanayofanya uwakala wa kusambaza matangazo katika vituo vya Televisioni
na Redio kusitisha kutumia takwimu za kampuni hiyo kama kigezo cha kutoa
matangazo kwa vituo vya Televisheni na Redio.
Aidha Dkt. Mwakyembe alifafanua
kuwa kama nchi haiwezi kwenda kwa utaratibu huu, kwani dunia ya leo ni
ya biashara na ushindani ni mkubwa ambao unaendana na kujiuza na
kujitangaza kwa chombo husika, hivyo alihoji “utajiuzaje kwenye soko
kama watu wanaotakiwa kubeba matangazo yako wanatoa taarifa zinazosema
kuwa wewe ni mdogo wakati ni mkubwa?.”
Dkt. Mwakyembe ameunda kamati ya
watu watatu inayohusisha Idara ya Habari (MAELEZO), Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
ambayo itafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wadau katika kikao hicho na
na mwishoni mwa mwezi wa kumi iwasilishe mapendekezo ya namna bora ya
ukusanyaji na usambazaji takwimu kwa mujibu wa sharia na taratibu.
Mmoja wa wachangiaji katika kikao
Bi. Basilisa Biseko kutoka vituo vya Radio na Televisheni alishauri
Serikali iweke viwango vya namna ya kufanya utafiti wa takwimu ambavyo
vitatumika na makampuni yote ya takwimu, lengo likiwa ni kuondoa
udanganyifu na kutofautiana katika taarifa mbalimbali za idadi ya
wasilikilizaji wa radio na watazamaji wa runinga.
Mweji Julai mwaka huu Ofisi ya
Taifa ya Takwimu iliizuia kampuni ya Geopoll yenye makao yake makuu
nchini Kenya kufanya tafiti za usikilizaji na utazamaji wa Redio na
Televisheni kwa sababu utafiti zao kushindwa kukidhi vigezo na masharti
ya ufanyaji tafiti hapa nchini.
No comments:
Post a Comment