Waziri wa sheria Dr Harrison Mwakyembe
Na kalonga kasati
Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk Harrisson Mwakyembe Ameitembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kusema kuwa ni Chombo Muhimu Ambacho Uwepo wake Unaipa heshima kubwa Tanzania kimataifa.
Akizungumza
katika ziara Aliyoifanya katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam Tarehe 31 Desemba 2015, Dk Mwakyembe Alisema Tume ni Chombo Muhimu kwa
taifa kilichoanzishwa kikatiba kwa lengo la kulinda na kutetea Haki za Binadamu Nchini.
"Wananchi Tunaowaongoza Wanakihitaji hiki Chombo kwa kuwa kimeundwa kusimamia Haki zao" Alisema Dk Mwakyembe
"Chombo
hiki kipo kwa Ajili ya kusimamia Masuala ya haki za Binadamu, Serikali Wakati mwingine katika kutekeleza majukumu yake yanaweza kutokea
mapungufu ya kiutendaji, ivyo Tume ipo kwa ajili ya kurekebisha Mapungufu hayo ili nchi iende vizuri" aliongeza
Dk
Mwakyembe Alisisitiza kuwa Tume inachokifanya ni katika Mipango ya
Serikali, na kwa Hakika inaisaidia Serikali iende katika Mstari Unaotakiwa.
Aidha,
Dk Mwakyembe Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wafanyakazi wa Tume kwa Uzalendo na Uadilifu Wao katika kazi Waliouonesha na Amewaahidi
kushirikiana Nao katika kutekeleza majukumu yao ya kila Siku.
Akizungumza Mapema, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Mheshimiwa Bahame Nyanduga Alimueleza Waziri, Dk Mwakyembe kuwa Pamoja
na Jitihada kubwa inayofanywa na Tume katika kuhakikisha inatekeleza Majukumu Yake ya kila Siku Bado inakabiliwa na Changamoto kubwa ya Rasilimali Fedha na Uchakavu wa Vitendea kazi.
No comments:
Post a Comment