Na Kalonga Kasati
Mahakama Kuu
Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya
ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa
mgombea ubunge katika jimbo Hilo kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema Highness Kiwia.
Katika
kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka 2015 iliyofunguliwa Novemba 25
mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga Ushindi wa mbunge wa Jimbo la
Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kutokana na
madai ambayo ni pamoja Na kuendesha kampeni za ubaguzi wa
kikabila sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga
kura walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Kesi
hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa mwanasheria wake Paul Kipeja
kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa Madai Ya kwamba mteja wake
ameshindwa kulipia gharama za Mahakama Ambazo ni Shilingi Milioni 10 na
kwamba washtakiwa walikuwa ni Angelina Mabula pamoja na Mwanasheria wa
Serikali ambapo Gharama ya kufungua kesi hiyo kwa kila mlalamikiwa
ilikuwa ni Shilingi Milioni Tano.
Kufuatia
ombi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Eugenia Gerald
Rujwauka alitoa maamuzi ya kuifuta kesi hiyo kama ambavyo mlalamikaji
alivyoomba.
Baada
ya kesi hiyo kufutwa, Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria
Mwandamizi aliekuwa akimtetea mlalamikiwa, amebainisha kuwa baada ya
maamuzi hayo anatarajia kukutana na mteja wake ili kujadiliana hatua za
kuchukua na huenda akafungua kesi ya madai dhidi ya Kiwia kutokana na
kufungua kesi na kisha kuiondoa mwenyewe na hivyo kumuingiza mteja wake
katika gharama zisizo za lazima.
Ifahamike
kwamba Angelina Mabula pamoja na Highness Kiwia Hawakuhudhuria
Mahakamani hapo na hakukuwa na Wafuasi Wengi wa vyama vya siasa kama
ilivyozoeleka ambapo nje
ya Mahakama hiyo, Agrey Laban ambae ni Katibu wa Kiwia Ameilalamikia
Mahakama kutokana na kushindwa kupunguza Gharama za kesi hiyo Jambo
ambalo limepelekea haki kupotea.
Wakati Hali ikiwa hivyo, Kheri James ambae ni Katibu wa Mbunge Wa Jimbo la
Ilemela Angelina Mabula, amepongeza maamuzi ya kesi Hiyo kufutwa na
kuongeza kuwa Hatua hiyo inatoa wigo wa Mbunge huyo
kuwatumikia wananchi.
Akiwa
ofisini kwake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu Akapata
fursa ya kuzungumzia Maamuzi ya Mahakama juu Ya kesi hiyo ambapo Amempongeza Mabula kwa uvumilivu wake kwa kuwa kiongozi akiwa na kesi
Mahakamani anakosa uimara wa kuwatumikia wananchi.
Katika
uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka jana, Angelina Mabula (CCM)
aliibuka mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kupata ushindi wa kura 85,425 na
hivyo kumshinda mpinzani wake Wakaribu kutoka Chadema Highness Kiwia
aliekuwa akitetea Jimbo Hilo ambae alipata kura 61,679.
No comments:
Post a Comment