TaarifaYa Ufafanuzi Kuhusu Malipo YaUmeme Kwa Askari Polisi
Katika Gazeti la Tanzania Daima Ukurasa wa 5, toleo Namba 4070 la Tarehe 25
Januari, 2016, lilichapisha habari yenye kichwa cha habari Polisi
“waisoma” namba. Sehemu ya Taarifa hiyo inaeleza kuwa askari Polisi hivi
sasa wanatakiwa kujilipia gharama za umeme.
Jeshi la Polisi nchini,
linakanusha vikali taarifa hiyo kwamba siyo sahihi. Ukweli ni kwamba Askari polisi wote makambini wanalipiwa umeme na serikali, ikiwemo wale
ambao nyumba Zao zimefungiwa luku kama njia ya kuboresha huduma na
matumizi sahihi ya umeme. Baada ya askari kununua umeme hutakiwa
kuwasilisha stakabadhi ya malipo ya umeme kwa ajili ya kurudishiwa kiasi
cha fedha walichonunulia umeme kila mwisho wa mwezi.
Aidha, habari iliyochapishwa na
Tanzania Daima ililenga kupotosha umma na mwandishi wa Habari hiyo
hakutafuta ufafanuzi kutoka kwenye mamlaka husika.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la
Polisi nchini, linamtaka mhariri wa gazeti la Tanzania Daima na
waandishi wake wa habari kuwa makini na habari wanazoziandika hasusani
taarifa Zinazohusu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuepuka madhara ya
kiusalama yanayoweza kutokea kutokana na habari wanazozitoa zisizo na
usahihi.
No comments:
Post a Comment