Mkuu wa Idara ya Huduma ya
Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond
Mwenesano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari leo jijini Dara es
salaam kuhusu Utaratibu mpya wa utoaji wa Huduma kwa wagonjwa wa nje
ambapo huduma zitakuwa zikitolewa kuanzia Jumatatu hadi jumamosi ikiwa
ni moja ya mikakati ya Hosipitali hiyo kuboresha huduma zake kwa
wananchi.
Afisa Uhusiano wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili Bi Neema Mwangomo akizungumza leo jijini Dar es salaam
wakati wa mkutano na Vyombo vya habari amabapo aliwataka Watanzania
kutumia huduma zinazotolewa na Hospitali hiyo ya Taifa kwa kuwa inao
wataalamu wakutosha kutimiza Jukumu hilo la kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya
Wagonjwa wa nje toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond
Mwenesano akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa Mkutano ulioenga kueleza mikakati ya Hosipitai hiyo katika
kuboresha huduma zake kwa Wananchi.kushoto ni Afisa Uhusiano wa
Hospitali hiyo Bi Neema Mwangomo na kushoto ni Muuguzi wa Hospitali hiyo
Bi June Samwel.
Na. Kalonga Kasati
Hospitali ya Taifa Muhimbili
imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili kupunguza Msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari Bingwa
kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Idara ya Huduma ya
Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Raymond
Mwenesano akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam amesema kuwa utaratibu huo
utawasaidia wagonjwa kupata huduma kwa Wakati na kupunguza Muda kusubiri Huduma.
Amesema Utaratibu huo utawahusu
wagonjwa wote wanakwenda kutibiwa katika Hospitali ya Muhimbili na
kuondoka hususan wale wanaolipa fedha taslimu na wale ambao ni wanachama
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bima za mbalimbali za Afya na
watumishi ambao makampuni yao yana mikataba na Hospitali kutibu
wafanyakazi wao.
Dkt. Mwenesano ameeleza kuwa
tayari Kliniki hizo zimekwisha anza kufanya kazi na kuongeza kuwa katika Hatua hiyo madaktari Bingwa pekee ndiyo watakaoona wagonjwa wakati wa
siku za kazi kuanzia saa 3 Asubuhi mpaka saa 12 jioni, pia jumamosi
kuanzia saa 3 asubuhi hadi za 8 mchana.
“ Muhimbili Tumeamua kufanya Mabadiliko haya kuanzisha Kliniki na kuwatumia Madaktari Bingwa peke
kwa lengo la kuboresha Huduma zetu, awali tulikuwa na Kliniki hizi
lakini huduma Zake zilikuwa hazitolewi kwa kiwango cha kuridhisha
kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha wa mdaktari hao kuhudumia
wagonjwa” Amesisitiza.
Aidha, Amefafanua kuwa Wagonjwa
wanaopatiwa Rufaa kuja hospitali ya Muhimbili wataendelea na Utaratibu
wa kawaida wa kwenda na Barua za Rufaa ili waweze kupatiwa huduma.
No comments:
Post a Comment