Na Kalonga Kasati
Bohari
Kuu ya Dawa (MSD), imesema iko kwenye Hatua Nzuri za kuanzisha Mradi wa Uzalishaji Dawa na vifaa Tiba Nchini kwa Ubia na Sekta Binafsi, lengo
likiwa kupunguza Tatizo la Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema Zabuni ya kumpata Mtaalamu Mshauri imekwishatangazwa Na inategemea kukamilika Mwezi huu.
Alisema,
kwa sasa Bohari huagiza kutoka nje ya nchi Dawa Na vifaa Tiba Takribani Asilimia 80 kutokana na Uchache na Uwezo Mdogo wa Viwanda vya ndani vya
kuzalisha Dawa na Vifaa tiba.
Bwanakunu
alisema, hali hiyo huilazimu MSD kuagiza Bidhaa zake kwa wingi kukidhi
mahitaji ya muda mrefu na Hivyo kulazimika kuwa na sehemu kubwa ya
kuhifadhia Bidhaa Hizo.
Akizungumzia Uwekaji Nembo kwenye Dawa za Serikali, Bwanakunu Alisema katika Mwaka
wa Fedha 2013/ 2014, MSD ilianza kuweka Nembo ya GOT ikimaanisha
Government of Tanzania (Serikali ya Tanzania).
Alisema,
nembo hiyo imewekwa kwenye vidonge, vifaa tiba na vitendanishi vya
maabara, kudhibiti kupelekwa kwenye Maduka Binafsi ya Dawa, badala ya
kutumiwa na walengwa Ambao wanatibiwa katika hospitali zinazosambaziwa
dawa Na MSD.
“Awali,
MSD ilikuwa ikiweka nembo ya MSD katika Vifungashio tu, Ambapo ilikuwa
ni rahisi dawa hizo kuhujumiwa na kwenda kusikostahili. Kwa kuweka Nembo Hiyo ya GOT pamoja na MSD katika Dawa, ni Hatua Mojawapo itakayosaidia
kupunguza ama kudhibiti kabisa Tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali,” Bwanakunu alisema.
Aliweka
wazi kuwa Hadi sasa asilimia 80 ya Bidhaa zimekwishawekewa nembo ya GOT
na kwamba wazabuni Wengine Wote Wanaopata zabuni za kupeleka Dawa
kwenye Bohari Hiyo Wanaelekezwa kuzingatia Utaratibu huo wa kuweka Nembo
ya GOT na MSD.
“Kufikia Juni 2016 Nembo ya MSD na GOT zitakuwa zimewekwa kwenye Bidhaa zote,” alisema Bwanakunu
No comments:
Post a Comment