Katika Maeneo ya Mkwajuni
Kinondoni Baadhi ya Wananchi Wamefunga Barabara Wanachoma Matairi kwa
kile wanachodai kupinga Bomoa Bomoa Askari wako eneo la tukio Wakijaribu
kuwazuia kufanya Matukio Hayo na Hakuna Magari Yanayoweza kupita Eneo
hilo Kutokana na Vurugu Zilizoababisha kufungwa kwa Barabara Hiyo ya
kutoka Moroco kwenda Magomeni.
MTU MMOJA MKAZI WA MADIBIRA WILAYANI MBARALI MKOA WA MBEYA AITWAYE KULWA BIDA [38] ALIUAWA NA WANANCHI WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUPIGWA MAWE NA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE BAADA YA KUTEREMSHWA KWENYE GARI LA LESAME KWA TUHUMA ZA KUMTOROSHA MTOTO AITWAYE KANG’WA MASUNGA [13] MKAZI WA MADIBIRA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
17.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:16 USIKU HUKO BARABARA YA MADIBIRA,
KUELEKEA MAFINGA, KATA YA MADIBIRA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI,
MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NI
BABA MKUBWA WA MTOTO HUYO NA ALIKUWA AKIMTOROSHA KWA LENGO LA KWENDA
KUMLEA. AIDHA KUTOKANA NA TUKIO HILO, WATUHUMIWA WAWILI WAMEKAMATWA
KUHUSIKA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. MAHELA MAGO [30] MKAZI WA IKOGA 2.
MASAYA MADENI [36] MKAZI WA NYAMAKUYU AMBAYE NI MLEZI WA MTOTO HUYO.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA
WENGINE ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA
RUJEWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI EMANUEL G.LUKULA ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUACHA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI.
TAARIFA ZA MSAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA
MKAZI WA MKANGE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE TUSAJIGWE MSHANE
[45] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI @ GONGO UJAZO WA LITA 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
17.01.2016 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MKANGE, KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA YA MTWIGA,
TARAFA YA KIPAMBAWE, WILAYA YA CHUNYA NA MKOA WA MBEYA.
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA
MKAZI WA MKANGE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA AITWAYE JAMES AYUBU [38]
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI @ GONGO UJAZO WA LITA 01.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 17.01.2016 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MKANGE, KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA YA MTWIGA,
TARAFA YA KIPAMBAWE, WILAYA YA CHUNYA NA MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
Imesainiwa na
[EMANUEL G.LUKULA – ACP]
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)Mhandisi Suleiman Said afariki dunia, Kuzikwa makaburi ya kisutu leo
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said
amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya
kuogelea,taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman
alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu,na baadae ikaelezwa kuwa
amekwishafariki na kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika leo. Marehemu
alipata kuwa Katibu mkuu wa Simba.
Taarifa zaidi zinasema Marehemu
Mr Sukeiman aliamka asubuhi akamwambia mke wake hajiskii vizuri, lakini
alienda baharini kuogelea kama kawaida yake. Walikuwa wawili na mwenzie,
wakaenda mbali sana wakati wa kirudi aliishiwa nguvu, alijitahidi
akafika nchi kavu akiwa hoi kabisa amekunywa maji wengi na akawa
anatokwa na mapovu mdomoni. Alifariki njiani akipelekwa hospitali. Msiba
upo upanga nyuma ya jeshi (Ngome) saa hii maiti imefuatwa wanakuja
kuaga hapa nyumbani, mwili utarudi msikitini saa tisa kisha kuzika
makaburi ya Kisutu nyuma ya chuo cha CBE. Apumzike kwa Amani.
Kinana alitakia heri Tamasha la Pasaka 2016
KATIBU Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amelitakia heri Tamasha la Pasaka la
mwaka huu linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions ambalo
litafanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza mwishoni mwa wiki,
ofisini kwake, Lumumba jijini Dar es Salaam, Kinana analitakia heri na
fanaka tamasha hilo na kumuomba Mungu aendelee kubariki utulivu na
mshikamano kwa Watanzania wote.
Kinana alisema Tamasha la Pasaka
lengo lake ni ujenzi wa Taifa letu na kudumisha amani na utulivu
tulionao sambamba na jukumu kubwa la kupiga vita umasikini na kuboresha
maisha ya Watanzania na kufikia kiwango cha juu cha maendeleo.
Kinana alisema Watanzania tuna
wajibu wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu na tuendelee
kusaidiana katika kila hali.
“Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe
ni muongozo wa kudumisha mshikamano na upendo miongoni mwetu ili
tuendelee kusaidiana katika kila hali,” alisema Kinana.
Katibu huyo alisema Watanzania
tunatakiwa kuzingatia hayo ili sote kuwa pamoja ili tupige hatua stahili
na kuondokana na umasikini uliokithiri.
No comments:
Post a Comment