Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw.
Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 2016. Majaliwa
amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini
Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli
kwenye mkutano wa SADC
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiweka saini kwenye kitabu cha
kumbukumbu mara alipowasili Mkoani Lindi kwa Ziara ya Kukagua miradi
inayotekelezwa na Wizara hiyo.Kulia ni ni Bi.Mariam Mtima Mkuu wa Wilaya
ya Ruangwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya Ujenzi wa
barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), kutoka kwa Mhandisi Mkazi
Anold Msengezi (Katikati) anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo juu ya Ujenzi wa
barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), ambapo amemtaka Mkandarasi
kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati na ubora unaokusudiwa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) akipokea taarifa
ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya (KM70.5) kutoka kwa Mhandisi
mkazi Dkt.Chaurasia inayojengwa na kampuni ya Jiangxi Geo Engineering
(Group) Cooperation ya China.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wakazi wa Nakapanya
alipopita kukagua bujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.5).
Sehemu ya barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
Na Mwandishi wetu
Tingatinga likiwa linaendela na
kazi za ujenzi barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi
wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka makandarasi wanaojenga
barabara za Mangaka-Mtambaswala KM 62.7 na Mangaka-Nakapanya Km 70,5
kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni mwaka huu.
Amewataka makandarasi hao kuongeza Rasilimali watu na vifaa ili
ujenzi huo ukamilike kama ilivyopangwa katika mkataba wa ujenzi wake.
“Hakuna muda utakaoongezwa nataka miradi yote miwili iwe
imekamilika ifikapo juni mwaka huu tena iwe kwenye ubora unaowiana na
thamani ya fedha,”amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Barabara hizo ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami ulianza
mwaka 2014 zitafungua fursa za kiuchumi mkoani Mtwara ikiwemo
kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja
lililoko Mtambaswala.
Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara
TANROADS mkoa wa Mtwara Eng. AISHA SALIM amesema hawata kubali maombi
yoyote ya kuongeza muda wa ujenzi wa barabara hizo ambapo ujenzi wa
barabara ya Mangaka –Mtambaswala Km 62.7 unatarajiwa kukamilika mwezi
Mei na ule wa Mangaka-Nakapanya KM 70.5 ukitarajiwa kukamilika mwezi
julai mwaka huu.
Mapema Prof. Mbarawa alikagua hali ya barabara wilayani
Ruangwa,Nachingwea na Masasi na kusisitiza kuwa ujenzi wa barabara na
madaraja katika wilaya hizo utaendelea katika kipindi kifupi baada ya
Serikali kuanza kutoa fedha kwa miradi inayotumia fedha za Mfuko wa
Barabara (RFB).
Waziri Mbarawa yuko katika ziara ya mikoa ya lindi na mtwara
kukagua miradi ya Barabara,Mawasiliano na Bandari ili kuona ufanisi
uliopo katika sekta hizo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment