SERIKALI YAKANUSHA UZUSHI UNAOENEZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUMHUSU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kaimu Mkurugenzi wa idara ya
Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa za
uzushi unaosambazwa katika mitandao ya Kijamii ya ndani na nje ya nchi
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Dkt. John Pombe
Magufuli amefukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanya biashara hapa
nchini kwa kuwa Serikali yake haitataki wageni wafanye bishara zao
nchini ambapo ukweli ni kwamba Serikali haijafukuza wageni wanaofanya
biashara zao nchini na haina mpango wa kufanya hivyo kwa wageni
wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Serikali.kushoto
ni Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya na
mwisho kushoto ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Isaac
Nantanga,Kulia ni Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.
Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara
ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya akitoa wito kwa Watanzania kuwafichua wale
wote wanaoingia na kuishi nchini kinyume cha sheria ili hatua stahiki
ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria na kanuni na kusisitiza kuwa
Ofisi yake itaendelea kufanya oparesheni ya kuwakamata watu hao, kulia
ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa na
Mwisho Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakifuatilia mkutano Idara ya Habari Maelezo kwa kushirikiana na Idara
ya Uhamiaji ukilenga kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji
zinasozambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Serikali imewafukuza
wafanyabiashara wakigeni wanaofanya kazi zao hapa nchini ,taarifa hizo
si za kweli na zinalenga kuichafua Serikali ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
Hivi karibuni kumejitokeza uzushi
unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ya ndani ya nchi na nje ya nchi
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli amefukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanyabiashara zao
nchini kwa kuwa serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.
Serikali haijafukuza wageni kutoka
nje ya nchi kufanya biashara nchini na haina mpango wa kuwafukuza
wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Idara ya
Uhamiaji.
Uzushi huo usiokuwa na ukweli
umeenezwa kufuatia Idara ya Uhamiaji kutekeleza jukumu lake la
kufuatilia wageni wote wanaoishi nchini bila vibali halali vya ukaazi
ambapo kwa mwezi Novemba na Desemba mwaka 2015 wageni 372 walioondoshwa
nchini.
Kazi ya kufuatilia wageni
wanaoishi nchini bila vibali halali vya kisheria haijaanza katika
Serikali ya Awamu ya Tano. Idara ya Uhamiaji nchini tangu Januari hadi
Desemba mwaka jana iliondosha nchini jumla ya wageni 1,642 waliokuwa
wanaishi na kufanya shughuli zao nchini kinyume na Sheria.
Uzushi unaoenezwa hauna ukweli
wowote na hauna nia njema na nchi yetu kwani kati ya mwaka 2014 na 2016
Idara ya Uhamiaji imetoa vibali vya ukaazi (Residence Permits) 40,765
kwa wageni wawekezaji na wafanyabiashara, wageni wanaofanyakazi za
kuajiriwa, wageni wanaokuja kwa ajili ya Masomo, matibabu, dini, utafiti
na wastaafu kuishi na kufanya shughuli zao nchini.
Serikali inawakaribisha wageni kuja nchini kuwekeza na kufanya shughuli zao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
Aidha, kuna uzushi unaenezwa kuwa
Rais Dkt John Pombe Magufuli amepiga marufuku wanawake kuvaa nguo fupi
kama njia ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Mheshimiwa Rais tangu aingie
madarakani hajawahi kuagiza wala kutoa tamko kuhusiana na uzushi wa
kukataza uvaaji wa nguo fupi ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi kama
inavyoenezwa katika mitandao ya ndani na Nje ya Nchi ambayo inanukuu
habari hiyo kuwa imeandikwa na Gazeti la Kenya “The Standard”
No comments:
Post a Comment