Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru Watanzania Wote, Wapenzi, na wadau Wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza Usiku saa 8 Uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es salam
kumpokea Mchezaji bora wa Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ndani Mbwana
Samatta.Samatta Alipokelewa na Viongozi wa serikali, TFF, familia yake Wakiwemo Baba na Mama yake mzazi na watanzania Wengi walijitokeza
kumlaki mchezaji huyo.Mara Baada Ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF
ilimpeleka moja kwa moja kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo Eneo
la Posta jijini Dar es salaam, ambapo imemlipia Gharama ya kukaa kwa
siku mbili.Akiwa hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda
alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Serikali, kisha Mchezaji alipata
nafasi ya kuongea na Waandishi wa habari.Kwa kuwa Jumanne, Januari 12 ni
Sikukuu ya Mapinduzi, na Janauri 13 ni fainali ya kombe la Mapinduzi
Visiwani Zanzibar, Siku ya Alhamisi Januari 14 TFF imeandaa dua Maalumu
ya kumpongeza Samatta itakayoongozwa na Viongozi wa Dini mbalimbali
katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11 jioni.Hata hivyo ratiba zingine
za kumpongeza Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa na Wadau Wengine
zinaweza kuendelea ilimradi TFF ijulishwe Mapema kwa Ajili ya kuratibu
uwepo wa Mchezaji Mwenyewe.
No comments:
Post a Comment