MAMLAKA ya Chakula na
dawa TFDA, imeaanza kutoa Elimu ya kula chakula salama kwenye shule Mbalimbali za mkoa wa Arusha ili kuwezesha wanafunzi na Jamii kuepukana
na Magonjwa ya maambukizi yanayosababisha vifo na Madhara Mengine ya
kiafya.
Meneja Wa Mamlaka ya Chakula na dawa TFDA, kanda ya
kaskazini, Damas Matiku, Amesema Elimu hiyo inayotolewa ikiwa ni Sehemu
ya Maadhimisho ya siku ya Chakula Dunani Ambayo imeanza Januari 19 na
kilele ni Januari 25 .
Matiko ,alisema Maadhimisho Hayo Yanawalenga zaidi Wanafunzi ambao ni Waathirika Wakubwa kutokana na kutokuzingatia kanuni
za chakula salama hususani kuangalia muda wa Vyakula Wanavyokula kama
matumizi yake yamekwisha mda wake.
Akielimisha Wanafunzi wa shule za Msingi Ekenywa na
Kiranyi, kwa pamoja wilayani Arumeru, Mkaguzi wa chakula na Dawa wa
TFDA, Barnabas Jacobo , amesema lengo la kutoa Elimu hiyo ni kulinda
afya za Walaji hasa Wanafunzi ambao ndio Waathirika Wakubwa wa Chakula
salama.
Amewaambia Wanafunzi hao kuwa wanapaswa kuishi kwa
kuzingatia kanuni za chakula ili Waepuke kupata Maambukizi ya magonjwa
mbalimba kama vile kuumwa na tumbo, kuhara, kuhara Damu, kutapika,
kuishiwa nguvu mwilini, homa ya matumbo, kichefu chefu,homa ya Bonde la
ufa, kifua kikuu, kimeta, minyoo ,kipindu pindu .
Jacobo,Ameongeza kuwa kupitia maadhimisho hayo wanafunzi na
jamii yakiwemo makundi Ya wafanyabiashara ya Matunda na mboga mboga,
pamoja na mama lishe watapatiwa elimu Hiyo ili waweze kuzingatia kanuni
sita za chakula na hivyo kuepuka kupata magonjwa ya kuambukiza.
Kwa upande Wao Walimu wa Shule za Msingi Kirenyi na
Enyuata, wameupongeza mpango huo Wa TFDA, wa kutoa elimu hiyo Muhimu na Utaongeza Uelewa zaidi kwa Wanafunzi katika kuzingatia kanuni za Chakula Salama.
Mkuu wa shule ya msingi Kiranyi Eliafile Issangya, amesema
mpango huo utasaidia kupunguza Magonjwa ya matumbo kwa wanafunzi na
walimu watatilia mkazo zaidi kufundisha uzingatiaji wa kanuni za chakula
.
Kwa upande wake mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi
Enyuata mwalimu, Simon Laizer , Alisema Elimu hiyo itasaidia kuelimisha
na kuzingatia uaandaaji wa vyakula salama hivyo kuondoa magonjwa ya
kuambukiza kwa wanafunzi .
Akizungumza Shuleni hapo kuhusu utekelezaji wa mpango huo
Afisa afya wa kata ya Kiranyi, Joseph Mpelumbe, amesema kuwa matumizi ya
vyoo katika kata hiyo na maeneo mengine ya wafugaji sio rafiki na bado
ni ya kiwango cha chini.
Alisema ofisi ya Afya ya kata
imejipanga kuanza kutumia sheria ili kuhakikisha kila mmoja Anakuwa na
choo na anakitumia hivyo kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na
kujisaidia hovyo na matokeo yake ni kueneza magonjwa.
No comments:
Post a Comment