Mwanasheria
mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
ametofautisha kilichomkuta Edward Lowassa kwenye Sakata la Richmond na
kilichomkuta Profesa Sospeter Muhongo kwenye Sakata la Escrow Bungeni.
Akiongea
katika kipindi cha Mada moto cha Channel Ten, Lissu alieleza kuwa kwa
kutumia ripoti za kamati za Bunge zilizomhukumu Lowassa mwaka 2008 na Ripoti za kamati ya Bunge ilizomhukumu Profesa Muhongo Mwaka 2014/2015
kuna utofauti mkubwa.
Alisema
kuwa ripoti ya Mwakyembe ilieleza kuwa Lowassa Anawajibika kwa makosa
ya watu watano wa chini yake Ambao aliwataja Majina na kwamba hakuna
sehemu ilimtaja Lowassa kuhusika moja kwa moja na sakata la Richmond.
Alisema
kuwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyokuwa chini ya
Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe, ilieleza Wazi kuwa Profesa Muhongo
alishiriki kudanganya kuwa Fedha zile hazikuwa za umma na baadaye
ikabainishwa na kamati hiyo kuwa zilikuwa fedha za umma.
“Kwa Mujibu wa kamati ya Mwakyembe, Lowassa aliwajibika kwa sababu ya Makosa
ya Hawa watu… Sasa hayo ni ya Lowassa. Yanalingana kiasi gani na ya
Profesa Muhongo, yanalingana kiasi gani na ya Profesa Muhongo aliyesema
kuwa bilioni 300 na ushee zilizotolewa Benki Kuu Zikagawanywa kama njugu
ni hela Binafsi.
“CAG
akachunguza akasema kuna Hela za Umma, Takukuru wakachunguza
hawajatuletea taarifa Bungeni mpaka leo. Bunge likachunguza likasema
hizi ni Fedha za umma na Hawa Watu wawajibike na wakawajibishwa. Kuna
ulingano Gani hapo? Na hapo nazungumzia Taarifa za kamati hizi Mbili za Bunge,” alisema Lissu.
No comments:
Post a Comment