Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa
Wilaya Morogoro Ameagiza polisi kuwakamata Wanakijiji wa Kisaki Stesheni Waliohusika na Mapigano kwa kutumia silaha za jadi jana tarehe
20/01/2016 katika Mkutano wa Hadhara uliyolenga kutoa Ufafanuzi wa Mgogoro huo.
Mkuu wa
Wilaya Bw.Muhingo Rweyemamu ameyasema hayo leo Alipokuwa Akizunguza kwa
njia ya simu Alipohitajika kutoa ufafanuzi kuhusu tukio la uvunjifu wa
amani kwa wanajikiji hao waliyokuwa na Mgororo Wa Ardhi unaowahususha Wakulima na Wafugaji.
“Mgogoro
huu wa Ardhi umesababishwa na Mwenyekiti wa Kijiji Bw. Ismail N’ganji
kwani aligawa ardhi Hiyo ya kijiji Mara Mbili kwa wakulima na wafugaji
wakati katika taratibu za kugawa Ardhi ni lazima Wanakijiji Waamue
katika kikao cha kijiji, na maombi ya kuomba ardhi ya Kijiji cha Kisaki
yalikuwa kati ya Wakulima na Wafugaji ambao kijiji kiliadhimia kuwa
ardhi hiyo ipewe wafugaji ambapo Mwenyekiti wa Kijiji Aliamua kugawa Ardhi hiyo kwa Wakulima kinyume na Makubaliano ya Mkutano wa Kijiji na
hapo ndipo Chanzo cha Mgogoro huo ulipoanza”, alisema Bw.Rweyemamu.
Mbali na
hayo Bw. Rweyemamu alisema mpaka sasa mwenyekiti huyo wa kijiji
ameshafukuzwa na uchaguzi Wa Mwenyekiti mwingine unatarajia kufanyika
hivi karibuni nakuwataka viongozi wa kijiji kuzingatia sheria Za Ugawaji
ardhi na kuacha kukiuka misingi hiyo kwani ndiyo inayosababisha
migogoro mingi ya ardhi katika Maeneo mbalimbali.
Akiendelea
kuzungumza mkuu huyo
Wa wilaya alisema Sheria ya Ardhi inaeleza vizuri
endapo mtu atahitaji ardhi isiyozidi heka 50 basi ni lazma Awasilishe Maombi hayo kwa Mkuu wa wilaya na Wanakijiji wahusishwe katika kikao cha
maamuzi ya kuridhia na kwa Upande wa mtu atakayehitaji Ardhi Zaidi ya
heka 50 basi Maombi yatatakiwa kuwasilishwa kwa Waziri wa Ardhi Nyumba
na Makazi.
Hata
hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo alisema Migogoro ya ardhi imekuwa
inasababishwa na Viongozi wa kijiji kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao
wamekuwa wakiendekeza Rushwa huku wakisababisha uvunjifu wa Amani kwa Wanakijiji hivyo wito wake ni viongozi hao Wazingatie Maadili ya
kiutendaji na kuachana na Vitendo vya Rushwa.
No comments:
Post a Comment