TRA yawaomba wananchi kutoa Ushirikiano
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba
wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa Taarifa za Maafisa wanaofanya kazi
kinyume na maadili.
Akiongea na mwandishi wa habari Wa Fofammedia hii leo
Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi
Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama
Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia Maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.
“Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara
ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa Taarifa Juu ya Maafisa wa TRA
wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.
Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa Taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi.
Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi
wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna Mwananchi atakayepata
tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.
TRA kupitia Idara yake ya Mambo ya Ndani
imepokea malalamiko mengi kutoka kwa Wananchi juu ya watumishi wa TRA
wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia Uchunguzi na Baadhi ya Watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.
Madaktari Bingwa Kutoka China Wakishirikiana NaMadaktari Wa Zanzibar Watoa Huduma Za MatibabuKwa Wananchi Wa Kijiji Cha Matemwe Unguja
Dokta
Abdull Maulid Abdull akimpima Miwani ya kuonea Mwananchi Chale Muumin
Fumu mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Tunda ngaa katika matibabu yalio
fanyika skuli ya matemwe mkoa wa Kaskazini unguja.
Dokta
Rajab Mohd Haj akimkagua Jicho Mzee Muhidin M Ali Mkaazi wa Kijiji cha
Matemwe katika matibabu yaliofanyika Skuli ya Matemwe Mkoa wa
Kaskskazini Unguja.
Dokta
Fei Jie kutoka China akimpima Masikio Bi Fatma Khamis Jaku mkaazi wa
Kijiji cha Matemwe Mfuruni katika matibabu yalio fanyika Skuli ya
Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Daktari
Bingwa kutoka China Yun Lai Gao kushoto na Mwanafunzi kutoka Zanzibar
School of Health Machano M Ali kwa pamoja wakipata maelezo kutoka kwa
Mgonjwa anaesumbuliwa na maradhi ya Ganzi Haji Ali Mcha kabla ya kumtibu
huko Skuli ya Matemwe.
No comments:
Post a Comment