Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi
George Pangawe akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)
kuhusu wananchi kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji nchini pale
wanapotaka kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni
Bi. Juliana Letara
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya
Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta akizungumza
na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu elimu ya uzalishaji na
matumizi endelevu ya rasilimali ili waweze kunufaika na rasilimali hizi
ambapo elimu hiyo imeingizwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kulia
ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na
Maendeleo ya Makazi George Pangawe.
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji,
Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara akisisitiza
jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Msaidizi
Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya
Makazi George Pangawe na kushoto ni
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta
Baadhi ya Waandishi wa Habari
wakifatilia mkutano uliondaliwa na, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Baraza la mazingira na Manispaa ya Kinondoni
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Kalonga Kasati
Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji
na matumizi endelevu ya rasilimali kwa wananchi ili waweze kunufaika na
rasilimali zote zilizopo katika maeneo yao kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es
salaam na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa
la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta wakati wa mkutano na Vyombo vya
Habari ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuelimisha umma
kuhusu Matumizi sahihi ya rasilimali ikiwemo Ardhi.
Akifafanua Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo
itawasaidia Wananchi kungamua na kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka
kutumia rasilimali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
’Elimu ya mazingira imejumuishwa katika
mitaala ya shule zetu hapa nchini ili kujenga uelewa kuhusu matumizi
sahihi ya rasilimali alisisitiza Mbuta
Akizungumzia faida za Elimu ya Mazingira
kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa itasaidia kujenga kizazi chenye
uelewa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuzingatia sheria na
kanuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw.
George Pangawe alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu zote za
kisheria pale wanapotaka kuendeleza Kipande chochote cha ardhi.
Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake
inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji wa Ardhi na kuwataka wananchi
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia Sheria na Kanuni
zinazosimamia Sekta ya ardhi.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mazingira pamoja na
Halmashuri zote nchini zimekuwa zikisisitiza kuhusu elimu ya uzalishaji
na matumizi endelevu ya rasilimali ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
No comments:
Post a Comment