Saturday, 30 January 2016

IMG_4361 (1024x683)Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.
IMG_4355 (1024x683)
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozungumza nao ofisini kwake.

Na Mwandishi wetu
WAZIRI mkuu, Majaliwa Kassimu Majaliwa, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ibada Maalum ya kumuingiza kazini askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania(KKKT),Askofu Dk Frederick Shoo katika kanisa kuu la Moshi mjini.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla,amesema Waziri mkuu anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) ambapo atapokea taarifa ya mkoa kabla ya kufanya shughuli za kanisa.
Alisema waziri mkuu hataongozana na waziri yeyote wa serikali ya awamu ya tano bali wasaidizi wake na baada ya ziara hiyo maalum atarejea Dodoma kuendelea na shughuli za serikali.
Ibada hiyo maalumu itajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro sanjari na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini,wadau wa maendeleo,waumini na Wananchi kwa ujumla.
Kutokana na ujio huo wa waziri mkuu, mkuu wa mkoa,aliwataka wananchi hususani katika wilaya za Hai na Moshi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye pia atapokea changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa
Kadhalika waziri mkuu anatarajiwa kutoa maelekezo ya serikali kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati anapewa taarifa ya mkoa.
Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa dayosisi ya Kaskazini amechaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa miaka minne na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake askofu Dk Alex Malasusa ambaye amemaliza muda wake wa uongozi.
Askofu Dk Shoo alichaguliwa mapema mwezi Agosti mwaka jana katika mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika chuo kikuu cha Tumaini jijini Arusha baada ya kuwashinda wenzake wawili.
Uchaguzi wa nafasi hiyo uliwashindanisha askofu Dk Stephen Munga wa dayosisi Kaskazini Mashariki na Askofu Charles Mjema wa dayosisi ya Pare.

 
Na Kalonga Kasati
Charles Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara
 
“Watanzania wengi wanakosa fursa mbalimbali zilizopo. Wengine wanakosa fursa za kibiashara pamoja na kazi kutoka katika Mashirika na Makampuni mbalimbali duniani kutokana na kushindwa kufahamu lugha za Kimataifa hususani kiingereza, Kijerumani, Kifarasa, Kichina na hata lugha nyingine. Hivyo niwasihi waamue kujifunza lugha, kwa kuwa lugha inafungua milango ya mafanikio maishani”. Anasema Mombeki.
 
Anasema, Watanzania wawaandae watoto wao katika lugha ya Kiingereza katika kupata elimu, akiunga mkono shule za watu ama Mashirika binafsi kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia, tofauti na ilivyo kwa shule za Serikali kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia katika shule za msingi akitanabaisha kwamba bado kiswahili hakijawa na nafasi kubwa kutumika kimataifa kama ilivyo kiingereza ambayo ni lugha inayowaunganisha watu wote Kimataifa. 
Mombeki anadokeza kuwa wanafunzi waliofundishwa kwa misingi ya kiingereza tangu wakiwa wadogo wana nafasi kubwa ya kufikia malengo yao ikilinganishwa na wale walioanza elimu yao ya  awali na msingi kwa lugha ya kiswahili.
 
Anabainisha kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka Mataifa ya Afrika, Amerika na Ulaya wanapenda kufika katika Centre hiyo ambayo ilianza kutoa elimu ya lugha mbalimbali tangu mwaka 1998. Pia inafundisha lugha ya Kiswahili pamoja na lugha za asili ikiwemo Kisukuma pamoja na Mila na Desturi za Tanzania.

No comments:

Post a Comment