Elimu ya sheria Dar kuanza Januari 31
Na Kalonga Kasati
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa
kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika
viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi
kupata elimu hiyo.
‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria
maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa
shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau
watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law
School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria
Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru
pamoja na Polisi.
Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao
watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo wananchi wenye mashauri
ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa
utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji,
Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka
katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam
inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.
Serikali kuendelea kujenga barabara zaidi kwa kiwango cha lami
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge
katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
Na Kalonga Kasati
Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha
lami ili kutatua adha kubwa ya Ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
lami ili kutatua adha kubwa ya Ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng Godwin Ngonyani
akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali
kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya
ubovu wa barabara nchini.
Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa
Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi
wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango
cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika mwaka wa fedha 2014/15
na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili
ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa
kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na
baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za Mradi huo, Serikali
itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele
Mwakibete Mbunge wa Busokelo (CCM) Aliyehitaji kujua ni lini barabara
ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia
Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi
Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani
amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa
kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10
Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha
lami na Ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae
Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa
Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi
Buseji,Wilayani Busokelo.
Serikali kupiti Wakala wa Barabara
(TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika
Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini ili kukabiliana na adha ya Ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya
maeneo.
No comments:
Post a Comment