Wabunge wa upinzani watoka tena bungeni leo
Wabunge wa upinzani wakitoka nje.
Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika vikao vya Bunge
vinavyoendelea mjini Dodoma baada ya wabunge wote wa upinzani leo kutoka
nje ya Bunge mara Baada ya wabunge kuanza kuchangia Hotuba ya Rais.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, yalifuata matangazo na
baada ya hapo wabunge walitakiwa kuanza kuchangia hotuba ya Rais
Magufuli lakini baadhi ya wabunge wa upinzani walianza kuomba Mwongozo
kuhusu kauli ya waziri mkuu kuhusu ishu ya michango ya chakula
wanayoendelea kulipishwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule za Bweni.
Hata hivyo, licha ya Baadhi ya wabunge wa Ukawa akiwemo Mbunge wa
Ubungo (Chadema), Saed Kubenea kuendelea kuomba mwongozo, naibu spika
aliwanyima nafasi hiyo, jambo lililosababisha Wasusie kikao hicho na
kutoka nje huku wakilalamika kwamba wamezibwa midomo.
No comments:
Post a Comment