Serikali kuanzisha Vyuo vya vya Uvuvi kuongeza ujuzi kwa vijana
Na Kalonga Kasati
Serikali imekusudia kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo
yote yanayozungukwa na bahari ili kuwafundisha vijana mbinu sahihi za
kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha kukuza vipato
vyao kwa kujiajiri.
Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate Ole Nasha
akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF)
kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani Lindi ili kuwaongezea
vijana ujuzi wa kazi hiyo.
Ameongeza kuwa wizara inatambua umuhimu wa kuwafundisha
vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi kilimo na ufugaji na
kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries
Education and Training Agency (FETA) imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani
Mtwara kwa lengo la kusogeza Huduma ya mafunzo ya uvuvi kwa wananchi
hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania ukiwamo mkoa wa
Lindi.
Mhe.William Tate Ole Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya
Uvuvi sio kwa maeneo Yanayozungukwa na bahari ila kwa maeneo mengine pia
ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio katika uvuvi pekee bali pia
katika kilimo na ufugaji, mbali na Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara Pia
kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani Mtwara chenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi Kigoma na Chuo cha Nyegezi
Mwanza.
Mbali za Vyuo hivyo serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania
nzima ili kuwawezesha vijana wengi Zaidi kupata kupata ujuzi zaidi
katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo na
kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo wanayapata.
Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa
mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka
2016/2017 na yale ya Astashahada na Stashahada yataanza mwaka
20017/2018.
No comments:
Post a Comment