BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatarajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippines mpambano wa raundi kumi wa ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title .
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
Kimweri Mpaka sasa amepanda
ulingoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa Ameshinda Michezo 14 na kupoteza michezo 3
Bondia huyo Mtanzania
anayefanya shughuli zake Australia amewaomba watanzania kumuombea Dua
kwa ajili ya mchezo wake huo ili afanye vizuri na kushinda Mchezo huo
ambapo baada ya hapo atakuwa na Uwezo wa kupigania Ubingwa wa Dunia wa WBA.
Kwa kuwa Maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni Mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana
Akishinda Mchezo
huo itabadilisha maisha ya mchezaji huyo wa masumbwi na kuwa na kipato
kikubwa Wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani
akianzia na mkanda wa WBA ambao Ameahidiwa kucheza Baada ya kushinda
mechi yake hii ya Feb. 26
Kimweri alitoa shukrani kwa
wadau wanaomsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya Nao kazi
ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwake katika
mchezo Wa Masumbwi, makocha hao ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka
yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila ‘Super D’
Kocha wa Tanzania Prison Remmy
Ngabo,Kameda Antony pamoja na Mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa
pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge
Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga
Ambao wamekuwa chachu kwake
katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo Alipofikia na
hata kama anaishi nje ya Tanzania amesema hawezi kusahau asili yake kwa
kuwa kitovu Tanzania ndipo kitovu chake kilipozikiwa.
No comments:
Post a Comment