Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akipeana Mikono na Balozi Wa Israeli nchini Mhe Yahel Vilan Alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 19, 2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Balozi wa Israeli nchini Mhe Yahel Vilan
Alipokutana na kufanya naye Mazungumzo Ikulu Jijini Dar es salaam leo January 19, 2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia Akiongea na
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Bw. Salman Bin
Ebrahim Al Khalifa katikati kuhusiana na maendeleo ya michezo nchini,
kushoto ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamali
Malinzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia Akiongea na
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Bw. Salman Bin
Ebrahim Al Khalifa kushoto kuhusiana na maendeleo ya michezo
nchini,katikati ni Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw.
Jamali Malinzi.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la
Soka Duniani (FIFA) Bw. Salman Bin Ebrahim Al Khalifa Katikati akiongea
na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.
Elisante Ole Gabriel kulia kuhusiana na maendeleo ya michezo nchini, wa
kwanza kushoto ni Rais Wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw.
Jamali Malinzi
Na Kalonga Kasati
SHIRIKA la Ugavi wa Umeme
Tanzania (TANESCO) limetolea Ufafanuzi kuhusu Malalamiko ya Wakazi wa
kijiji cha Seseko Kata ya Mwamalili mkoani Shinyanga.
Ufafanuzi huo Umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bw. Lusajo
Mwakabuku Wakati Akiongea na Idara ya Habari mara baada ya kuhojiwa
kuhusu madai ya Wakazi wa kijiji hicho kuhusu kufyekwa kwa mazao yao
bila ya kulipwa fidia na Shirika hilo.
Mwakabuku Amefafanua kuwa madai
ya wakazi wa eneo hilo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara licha ya
TANESCO kuwalipa fidia kwa wakazi hao tangu mwaka 1999.
Mwakabuku
amefafanua kuwa, Madai hayo yanatokana na njia ya msongo wa Umeme wa
kilovoti 220 ambayo ni njia inayotokea Shinyanga kuelekea Mwanza na
inaonekana hawa wanaolalamika kufyekewa mazao yao ni wale ambao
wamevamia ama wameweka makazi yao hivi karibuni katika Maeneo hayo
kwasababu Shirika la TANESCO lilishawalipa wakazi ambao walipitiwa na
nguzo hizo tangu mwaka 1999.
Aidha, Bwana Mwakabuku aliongeza kuwa, TANESCO kabla ya kupitisha nguzo katika maeneo ya makazi ama mashamba ya Wananchi huwa Wanawasiliana na Uongozi wa eneo Husika na kukubaliana na wananchi wenyewe ili waruhusiwe kupitisha ama kutopitisha Nguzo za Umeme, na ilipotokea Wanakubaliwa Basi fidia inalipwa kwa Wakati na kwa kufuata utaratibu ikiwemo kufanya Tathmini ya kutosha na kisha kuwalipa kwa Wakati kulingana na Matakwa ya Sheria.
‘’Wakati Mwingine Baadhi ya Wananchi wamekuwa wasikivu kwa kukubali na kuruhusu kupitisha Nguzo za Umeme katika Maeneo yao na Tumekuwa Tukiwalipa fidia, lakini kuna Wengine Wamekuwa wakifanya Shughuli za kibinadamu ikiwemo ulimaji mazao chini ya laini za umeme kwa Makusudi ili walipwe fidia pindi yakifyekwa, Hawa Wanakuwa wanavunja Utaratibu ambao Umewekwa na TANESCO kuwa, ndani ya mita thelathini kwa pande zote mbili ambazo laini Zinapita hakutakiwi kufanyika shughuli yoyote ya makazi au maendeleo, hivyo katika ukaguzi Wetu tunapofika na kukuta wamekiuka taratibu hizo tunazuia uendelezaji wa shughuli hizo na hasa kubwa likiwa ni suala la Usalama wa Mali na Maisha yao Wenyewe wananchi.’’, alisema Mwakabuku.
Amewahasa wakazi nchini kote kuzingatia Sheria ya mita 60 kwa kutofanya shughuli zozote za kibinadamu chini ya Nguzo za umeme kwa ajili ya usalama wa maisha yao kwani umeme upitao Unakuwa ni wa Msongo Mkubwa hivyo unaweza kuhatarisha maisha yao endapo wanakaidi kufanya hivyo.
‘’Napenda kusisitiza kuwa, Wananchi wazingatie na kuhakikisha kuwa hawafanyi shughuli zozote Za kiuchumi au Ujenzi wa makazi Ndani ya eneo la mita 60 kutoka kilipo chanzo cha umeme ili kuondoa kero na madai kama haya’’, alisisitiza Mwakabuku.
Na Kalonga Kasati
Mwenyekiti wa Good News for All
Ministry, Askofu Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kujitokeza
kumuomba Mungu dhidi ya hali ya hewa ya joto kali nchini.
Askfou huyo Ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar e s Salaam
mara Baada ya Mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha hali ya joto kufika
nyuzi joto 35°C.
Askofu Gadi ameongeza kuwa,
wanatarajia kufanya mkutano wa maombi siku ya Jumatano ya Tarehe 20
Januari mwaka huu katika eneo la Soko la Samaki maarufu kama Feri ili
kuomba Mungu kuepusha ongezeko la joto nchini.
“Joto limesambaa katika maeneo
ya pwani hususani Dar es Salaam, Tanga, na visiwa vya Zanzibar, hivyo
kwa hali hii tumeona tufanye mkutano wa maombi mafupi katika eneo la
Soko la samaki la feri siku ya Jumatano kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6
mchana,
“Mungu Amenipa nafasi ya kuomba
dhidi ya majanga ya kimazingira kama haya hivyo Tunawakaribisha watu
wote wa Dar es Salaam tuje tumlilie Mungu kwa pamoja ili tuondokane na Janga hili la Joto na Madhara ya Elnino” alifafanua Askofu Gadi.
Kwa upande wake katibu wa Good
News For All Ministry Mchungaji Palemo Massawe Amewataka Wananchi
kuchukua hatua ili kujikinga Dhidi ya Ugonjwa wa kipindupindu kwa
kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka.
Uongozi huo Unaendelea na
maombi ya kumuombea Rais John Pombe Magufuli kufanikiwa katika juhudi
zake za kulikomboa nchi kiuchumi na kielimu.
No comments:
Post a Comment