Waziri Mkuu kassim Majaliwa
Na Mwandishi wetu
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa leo Ataanza Ziara ya siku Tatu Mkoani Ruvuma,
kuhimiza Na kukagua Shughuli Mbalimbali za Maendeleo. Hayo Yamesemwa na
Mkuu wa Mkoa, Said Mwambungu Alipozungumza na Waandishi wa Habari
ofisini kwake Mjini Songea
Alisema,
Waziri Mkuu Atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea saa 6 Mchana,
ambapo Atapokelewa na viongozi wa Serikali na vyama vya Siasa. Mwambungu Alisema Atakapowasili Mjini Songea, Waziri Mkuu Atakwenda Moja kwa moja
Ikulu Ndogo kisha kusomewa Taarifa ya Mkoa.
Kesho
asubuhi Waziri Mkuu atafungua Benki ya Posta Tawi la Songea na
kutembelea Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mjini Songea, Ambapo Atakagua
kila kitengo na kuzungumza Na Wafanyakazi wa Hospitali. Pia Waziri Mkuu Atazungumza na Watumishi wa idara zote za Serikali Waliopo Mjini Songea.
Mwambungu Alisema Baada ya kumaliza kuzungumza na Watumishi Hao, Atatembelea
Kitengo Cha Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na kukagua Maghala Yanayotumika kwa Ajili ya kuhifadhi Chakula.
Aidha, Atatembelea kuona ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya
Songea Vijijini katika kijiji cha Lundusi kata ya Maposeni na kuzungumza
na Wananchi katika Mkutano wa Hadhara. Mkuu Huyo wa Mkoa Alisema
keshokutwa Waziri Mkuu Atafanya Majumuisho ya ziara Yake Mjini Songea.
Mwambungu Aliomba Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika Maeneo yote ambayo Waziri
Mkuu Atatembelea, ikiwemo barabarani, ili kumlaki. Hii itakuwa ni Ziara
ya Pili ya kiserikali Ya Waziri Mkuu, Tangu Alipoteuliwa kushika Wadhifa.
Wiki
iliyopita Alikuwa mkoani Kigoma, Alikotembelea Miradi Mbalimbali na
kukutana Na Wafanyakazi wa idara Mbalimbali za Serikali, kufanya Mikutano ya Hadhara na kuzungumza na Wananchi.
Akiwa Huko, Waziri Mkuu Majaliwa Alibaini kuwepo kwa Ubadhirifu Wa Fedha za
umma, Unaohusisha Uuzwaji Wa Jengo la Shirika la Maendeleo Kigoma
(KIGODECO) kwa Bei ya kutupwa.
Majaliwa
alitoa siku mbili kwa Katibu Tawala Wa Mkoa wa Kigoma, Dk John Ndunguru
kukamilisha Uchunguzi Wake na kumpatia Taarifa ya Maandishi Juu ya Tuhuma za Ubadhirifu Huo.
Aliagiza
pia Uchunguzi Juu ya uuzaji wa viwanja 12 vya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Unaodaiwa kukiuka Taratibu. Alitoa Maagizo Hayo Desemba 30, Mwaka Jana Wakati Akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo, Alipokuwa Akifanya Majumuisho ya ziara yake ya siku mbili.
No comments:
Post a Comment