Na Kalonga Kasati
Mamalaka ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu Na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya Maoni ya Wananchi Juu ya Viwango vya Nauli Za Mabasi Yatakayotoa Huduma ya Usafiri wa Haraka Jijini Dar es Salaam.
Mamalaka ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu Na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya Maoni ya Wananchi Juu ya Viwango vya Nauli Za Mabasi Yatakayotoa Huduma ya Usafiri wa Haraka Jijini Dar es Salaam.
Taarifa
hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Wa SUMATRA kwa vyombo vya Habari
kwenda kwa Wananchi Ambapo ofisi hiyo itawaalika Wadau Wote wa Usafiri
hususani Wananchi kuchangia Maoni kwenye Mkutano Utakao fanyika Januari 5
kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na Nusu
asubuhi.
Mamlaka
pia inapokea Maoni ya Wananchi kupitia Anuani ya ofisi ya Mkurugenzi
Mkuu Wa Mamlaka hiyo ambayo ni S.L.P 3093 au kwa Barua pepe ambayo
info@sumatra.go.tz Ambapo kabla ya kufikia Uamuzi Wadau Wanatakiwa kutoa Maoni ya kuridhia viwango Vya Nauli kwa Mujibu wa Sheria ya Sumatra.
Maoni
ya Maandilizi Yatapokelewa kwenye Ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo
la Mawasiliano House Makutano ya Barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo
kuanzia Saa 4 Asubuhi Hadi saa 9 alasiri Mwisho wa kupokelewa Maoni
hayo ni Januari 13 Mwaka Huu
Mamlaka Hiyo imepokea Maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa Huduma ya Mpito ya Usafirishaji Jijini Dar es Salaam katika kutekeleza Awamu ya kwanza Ya Mradi wa Dart.
Maombi Yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni Safari kwenye Njia za pembeni
(feeder route) Shilingi 700 ,Safari kwenye njia kuu (trunk route)
shilingi 1200 na Njia Zote Mbili ni 1400 Ambapo Wanafunzi Watalipa Nusu Nauli Anayotoa Mtu mzima.
No comments:
Post a Comment