Thursday 18 June 2015

Ajali Arusha: Trafiki Saba, wanasurika kifo, gari la Polisi lagongwa


Ni baada ya dereva kusimamishwa akakataa, Trafiki wakapiga simu mbele, alipofika akakutwa askari wameweka kizuizi njiani akawagonga.

Taarifa zisizo rasmi watatu wamefariki hapo hapo
Askari saba wanusurika kifo baada ya gari yao kugongana na gari ya utalii mkoani Arusha





Askari saba wa Jeshi la Polisi nchini, kitengo cha Usalama Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali iliyohusisha gari la Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.

Gari zilizohusika katika ajali hiyo, zote ni aina ya Toyota Land Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la Polisi nchini, na jingine lenye namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya kampuni moja ya Utalii mkoani humo.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kupitia taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa kijamii unaoendeshwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo imesomeka kama ifuatavyo;

Ni kweli ajali imetokea na kusababisha majeruhi 7 wakiwa ni askari wa U/barabarani Arusha. Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva hatimaye kushindwa kumudu gari na kusababisha gari kuhama lane nyingine na kugonga gari la Polisi lililokuwa linakuja mjini Arusha. Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospita kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment