Wafuasi wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanaandamana nje ya mahakama kuu
mjini Nairobi, wakiitaka tume ya kitaifa inayoajiri na kufuatilia
mienendo ya majaji iwachunguze.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Twitter wa gazeti la kibinafsi la Daily Nation,
Wafuasi wa Kenyatta wamekusanyika wakiwashutumu majaji wa mahakama kuu
kwa kuwaibia "ushindi wao ".
Majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wa kubatilishwa kwa matokeo ya
uchaguzi wa urais wa tarehe 8 Agosti yaliyompatia ushindi Bwana Kenyatta
baada ya kusema kuwa mchakato wake ulitawaliwa na "ukiukaji wa sheria
na makosa"
Maandamano hayo yamefanyika wakati gazeti la The Standard kuchapisha
taarifa ya madai kwamba majaji wawili wa Mahakama kuu , Philemona Mwilu
na Isaac Lenaola, ambao walipigia kura kubatilishwa kwa uchaguzi,
walikutana na mawakili wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati wa
kusikilizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wa Bwana Uhuru Kenyatta.
Taarifa hiyo iliyotawala mazungumzo ya raia wa Kenya kwenye mtandao wa
Twitter,pia inasema kuwa kuna mazungumzo ya simu yaliyo rekodiwa
kuthibitisha kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya majaji na mawakili
wa upinzani waketi kesi hiyo ikiendelea.
mwandishi wa habari nchini humo ameripoti kuwa waandamanaji wamekwisha
wasilisha madai yao kwa tume ya huduma za mahakama inayowaajiri na
kuchunguza mienendo ya majaji nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment