Friday, 1 September 2017

Ukuta utakaojengwa mpakani mwa Marekani na Mexico

Utawala wa rais Donald Trump umechagua makampuni manne kwa kazi ya kujenga sampuli ya ukuta ambao rais Trump ulitangaza sana juu ya mpaka wa Mexico na nchi yake.
Ukuta huo ulikuwa ni miongoni mwa vipaumbele vya kwanza vya rais Trump na kuzusha sintofahamu na kusababisha maandamano pande zote mbili.
Naibu Kamishna Ronaldo Vitiello,ambaye pia ni mkuu wa doria katika mpaka wa Marekani amewaambia waandishi habari kwamba mikataba ya ujenzi wamepatiwa makampuni kutoka Alabama Arizona, Texas na Mississippi.
Inaelezwa kuwa gharama halisi za ujenzi huo zinakadiriwa kuwa hadi dola milioni unusu. Wakati wa kampeni zake rais Trump amesisitiza kwamba Mexico watalipa gharama ya ukuta huo. Sampuli hiyo ya ukuta itajengwa mjini San Diego, California.

No comments:

Post a Comment