Aina ya Treni za ‘Flying Train’
Kampuni ya Makandarasi kutoka China ya Aerospace Science and Industry
Corporation (CASIC), ipo mbioni kuanza ujenzi wa mradi wa treni za juu
(Flying Train) zitakazokuwa na kasi kubwa kuzidi ile ya mwanga na sauti.Treni hizo ambazo zitakuwa zinasafiri kwenye bomba maalumu (vacuum tube) lililotegwa juu ya nguzo zitasafiri umbali wa kilometa 4000 kwa saa na kwa spidi hiyo zitakuwa ndio chombo cha kwanza cha usafiri kuwa na mwendo kasi zaidi duniani.
Muonekano wa Treni utakavyokuwa kwenye reli yake iliyofungwa bomba maalumu lenye vioo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Liu Shiquan amesema bado wanafanya utafiti kuangalia ni jinsi gani mradi huo utafanikiwa ili kupunguza kupunguza adha ya usafiri nchini china na nchi nyingine za bara la Asia.
“Tunaona dunia inakwenda kasi kwenye teknolojia watu wamechoka kutumia muda mwingi kwenye usafiri nadhani tunahitaji kufikiria zaidi kwani watu wanaongezeka na mahitaji yanaongezeka,“amesema Liu Shiquan kwenye mahojiano yake kwa lugha ya kichina na gazeti la The Paper.
Treni hizo ambazo zitaendeshwa kwa kutumia nguvu ya sumaku umeme zitaenda kwa kasi mara 10 ya treni za sasa ambazo zinaenda kasi zaidi duniani kwa kilometa 300 zilizozinduliwa mwaka huu nchini humo.
“Najua kusafiri kwa kasi kubwa zaidi inaogopesha lakini hatuna budi kufanya hivyo kwani wapo watu wengine watakuwa wametimiza ndoto zao, ingawaje itakuwa ni gharama kubwa kusafiri”,amesema Mkurugenzi Mkuu kitengo cha Usanifu wa kampuni ya (CASIC), Bwana Mao Kai.
Treni hizo zitaanza kazi nchini China na baadae kusambaza reli kwa nchi 70 zilizosaini mkataba wa OBOR zikiwemo nchi kutoka barani Ulaya na Afrika.
Kuhusu ni lini mradi huo utakamilika Bwana Mao Kai amesema bado hadi watakapokamilisha tafiti zao ila mradi unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni $500.
No comments:
Post a Comment