Saturday, 2 September 2017

Mourinho na ndoto ya Ubingwa

Kocha wa Man Utd, Jose Mourinho.

HABARI ya mjini sasa ni Manchester United, kwani imekuwa na mwanzo mzuri katika msimu wa Ligi Kuu England wa 2017/18 chini ya Kocha Jose Mourinho. Hadi sasa Man United imecheza mechi tatu na kushinda zote, imefunga mabao kumi na haijafungwa hata bao moja, huu ni mwanzo mzuri kwa klabu kama hii. Upande mwingine ni kwam
b Man United msimu uliopita iliishia kushika nafasi ya sita, lakini msimu huu itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani ilitwaa ubingwa wa Europa League msimu uliopita.
Licha ya kumaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita na kutwaa ubingwa wa Europa League, Man United pia ilitwaa ubingwa wa Kombe la Ligi na Ngao ya Jamii na kufufua matumaini ya kufanya vizuri. Tangu Kocha Sir Alex Ferguson aondoke ni misimu minne imepita ambapo tangu 2013, Man United imeweza kushika nafasi za saba, nne, tano na nafasi ya sita msimu uliopita. Msimu huu Man United imeanza vizuri kwa kuzifunga West Ham United mabao 4-0, Leicester City mabao 2-0 na Swansea City mabao 4-0.
Pamoja na kuanza vizuri msimu huu, hapa chini ni baadhi ya mambo yanayoifanya Man United kuweza kutwaa ubingwa wa Premier League msimu huu;

USAJILI MPYA
Usajili mpya wa Man United unamjumuisha Romelu Lukaku, huyu ni straika aliyesajiliwa kutoka Everton, amethibitisha yeye ni mfungaji na anaijua kazi yake. Katika mechi tatu hadi za ligi kuu amefunga mabao matatu. Lukaku alisajiliwa kuchukua nafasi ya Zlatan Ibrahimovic ambaye ni majeruhi wa goti, hata hivyo Zlatan naye ameongezewa mkataba mpya, hivyo mziki umekamilika.

Kuna msemo unaosema, “Mabao yatakufanya ushinde mechi, beki bora itakupa mataji”, usemi huo umejidhihirisha kwa Man United kwani licha ya kumsajili Lukaku, pia imewasajili beki wa kati Victor Lindelof na kiungo mkabaji Nemanja Matic. Hao wote ni watu wa kazi.

UWIANO MZURI

Leicester City iliweza kutwaa ubingwa wa England mwaka jana kutokana na uwiano mzuri wa kikosi chake kuanzia golini, mabeki, viungo na washambuliaji.

Pamoja na kuanza vizuri msimu huu, hapa chini ni baadhi ya mambo yanayoifanya Man United kuweza kutwaa ubingwa wa Pre Usajili mpya wa Man United unamjumuisha Romelu Lukaku, huyu ni straika aliyesajiliwa kutoka Everton, amethibitisha yeye ni mfungaji na anaijua kazi yake.

Paul Pogba
Katika mechi tatu hadi za ligi kuu amefunga mabao Lukaku alisajiliwa ku-Upande mwingine ni kwamba, Man United msimu Lukaku alisajiliwa ku chukua na Leicester langoni ilikuwa na Kasper Schmeichel, mabeki wake Wes Morgan na Robert Huth walikuwa poa na kiungo wao mkabaji N’Golo Kante na mbele ilikuwa na Riyad Mahrez na Jamie Vardy, hakika kilikuwa kikosi bora.
 Sasa msimu huu Man United nayo imetulia kuanzia langoni kwa David de Gea, na usajili wa Lindelof na Matic. Pia wapo Eric Bailly, na Antonio Valencia.

Uwepo wa Henrikh Mkhitaryan, Juan Mata, Anthony Martial na Paul Pogba unaifanya timu hiyo kuwa imara. Lukaku, Rashford na Zlatan pia wanachagiza uwiano mzuri wa ushambuliaji kwa Man United msimu huu ndiyo maana katika mechi tatu wamefunga mabao kumi bila kufungwa.

POGBA YUPO

Paul Pogba msimu uliopita alikuwa ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kuliko mwingine yeyote akiwa amesajiliwa kutoka Juventus kwa dau la pauni milioni 89.3.

Licha ya Neymar kuweka rekodi mpya msimu huu kwa kusajiliwa kwa zaidi ya pauni milioni 190 kutoka Barcelona kwenda PSG, bado wengi wanasubiri kitu kikubwa kutoka kwa Pogba. Msimu uliopita Pogba alionyesha vitu vyake na kuishia kuipa mataji timu yake, hivyo msimu huu anaweza kuwa sababu ya Man United kutwaa ubingwa wa Premier kwani sasa amepevuka na anaijua vizuri ligi ya England.

Uwepo wa Matic katika kiungo, kunamfanya Pogba awe huru zaidi kucheza anavyoweza tofauti na msimu uliopita. Pasi zake, mashuti langoni na ule unyumbulifu wa kucheza nafasi nyingi ni faida kwa kuwa na Pogba.

HALI YA USHINDI

David De Gea ni mmoja kati ya wachezaji wa sasa wa Man United waliowahi kutwaa ubingwa wa Premier huko nyuma. Kihistoria, Man United ilikuwa imara ikiwa na kikosi chenye ari kubwa ya ushindi chini ya Koc h a Sir Alex Ferguson kiasi kwamba mashabiki wake hawakuwa na presha juu ya ushindi.

Hata hivyo, ari hiyo iliondoka mwaka 2013 baada ya Ferguson kuondoka na hadi msimu uliopita hali ilionekana kuwa ngumu kwa Man United kutwaa mataji lakini sasa mambo yanaonekana kuwa vizuri.

Tazama kikosi cha sasa kimebakiwa na De Gea, Valencia, Michael Carrick, Chris Smalling, Ashley Young na Phil Jones ambao walitwaa taji kwa mara ya mwisho, lakini kati yao ni De Gea na Valencia tu wanaopata nafasi kikosi cha kwanza sasa hivi. Ubingwa wa Europa League na Kombe la Ligi msimu uliopita, umeifanya Man United kuwa na hari ya ushindi hadi sasa. Katika usajili mpya, Matic katoka Chelsea na alitwaa ubingwa Premier msimu uliopita na hata Lindelof alitwaa ubingwa wa Ureno na Benfi ca.

MSIMU WA PILI KWA MOURINHO

Huu ni msimu wa pili kwa Kocha Jose Mourinho na ana dira ya kutwaa ubingwa ukitazama kikosi chake hata rekodi zake za h u k o nyuma.

Amejiandaa vizuri kabla ya msimu huu kuanza, lakini rekodi zinasema, Mourinho alitwaa ubingwa katika msimu wa pili wakati akizifundisha FC Porto, Chelsea (mara mbili), Inter Milan na Real Madrid. Mourinho sasa anakijua ipasavyo kikosi chake na vikosi vya timu pinzani hivyo msimu huu kazi yake ni rahisi ku

liko msimu uliopita ambapo alikuwa akihangaika kupata matokeo. Ukikitazama kikosi cha sasa cha Man United, uchezaji wake unaonyesha timu ipo tayari na ina njaa ya kutwaa ubingwa tena siyo wa Pre
mier tu hata Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MADOGO WAKALI
Msimu uliopita ulikuwa mgumu kwa Man United kwani kuna wakati ilicheza mechi kila baada ya siku tatu. Ikalazimika kuwatumia baadhi ya chipukizi wake, sasa chipukizi hao wameimarika.

Chipukizi kama Marcus Rashford, 19, na Anthony Martial, 21, wameonyesha kuimarika sasa na wote wana hamu ya kuwa nyota wa dunia. Wote hao wanaweza kufanya lolote dakika yoyote kwa beki yoyote ile. Rashford alitoa asisti kwa Lukaku dhidi ya West Ham huku Martial akihitaji dakika 15 tu za kufunga au kutoa asisti. Ukitazama beki yake, Eric Bailly na Victor Lindelof wote wana miaka 23 hata Pogba ana miaka 24 tu.

WAZOEFU WAKALI
Usajili wa Matic, umeifanya Man United kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji wakongwe na wenye uzoefu ambao wanaweza kutwaa ubingwa mara kadhaa, hao wametwaa mataji kibao.

Wachezaji kama nahodha Michael Carrick, Antonio Valencia, David de Gea, Chris Smalling, Juan Mata, Victor Lindelof, Ashley Young hata Pogba, hawa wote wameshatwaa mataji kibao. Mtazame Matic, huyu ana mataji mawili ya Premier akiwa na Chelsea ndani ya miaka mi- tatu tu iliyopita. Taji la Europa League msimu uliopita, pia linawapa nguvu wazoefu hawa kutwaa ubingwa wa
ligi kuu.

No comments:

Post a Comment