Picha na OMR
Serikali imesema awamu ya pili ya Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma itaanza rasmi Julai mwaka huu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema
zabuni kwa ajili Ya ujenzi zitatangazwa badae mwaka huu ili kuuwezesha
Uwanja huo kuwa na hadhi ya kimataifa Na kuchochea fursa za utalii
katika ukanda wa Magharibi na Mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Zaidi
ya Shilingi Bilioni 40 kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB),
zinatarajiwa kutumika Hivyo kuwataka wananchi ambao eneo lao liko katika
Uwanja huo kuondoka mara moja mara baada ya kulipwa fidia.
“Nia
ya Serikali ni kuongeza njia ya kuruka na kutua ndege kutoka urefu wa
mita 1800 sasa hadi Mita 3100 na hivyo kuruhusu ndege kubwa aina ya
Boeing 737 kutua katika uwanja huo”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amewataka wananchi wa Kigoma kutoa ushirikiano mkubwa kwa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili zoezi la
ujenzi lifanikiwe kwa haraka na kuepuka vikwazo vinavyoweza kuchelewesha
mradi huo.
Naye
Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amewataka wananchi wa Kigoma na
wawekezaji kujipanga kutumia fursa ya uwanja huo kuwekeza ili kukuza
sekta ya utalii na usafirishaji katika Mwambao wa Ziwa Tanganyika pindi
uwanja huo utakapokamilika.
“Tuna
bahati kupata Serikali inayowekeza katika mkoa wa Kigoma, nawaomba wana
Kigoma Wenzangu tuepuke migogoro na kutumia fursa hii kuwekeza
kikamilifu ili kukuza utalii katika Ukanda wa Magharibi na kuongeza
mapato katika mkoa wa Kigoma”, amesisitiza Mhe. Zitto.
Amemhakikishia
Profesa Mbarawa kuwa Uwanja wa Ndege wa Kigoma utafungua usafiri wa
Anga kwa ukanda wa magharibi na nchi jirani na hivyo kuongeza idadi ya
watalii na watumiaji wa usafiri wa anga katika mwambao wa Ziwa
Tanganyika, hifadhi za Taifa za Gombe na Mahale na mikoa ya kanda ya
magharibi.
Kwa
upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkoani Kigoma Bw.
Godlove Longole ameiomba Serikali kukamilisha Ujenzi wa uzio, Jengo la
Abiria, Mnara wa kuongozea Ndege na huduma za zimamoto katika uwanja huo
ili kuuwezesha kufanya kazi zake kwa viwango vinavyotakiwa.
Meneja
wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma Bw. Mohamedi Issa amemhakikishia Waziri
kwamba Atasimamia mchakato mzima wa mradi wa ujenzi kwa uadilifu,
uaminifu ili thamani ya mradi huo iwiane na ubora wa kazi itakayofanywa
na hivyo kuuwezesha uwanja huo kufikia kiwango cha Code 4C
kinachowezesha ndege zenye ukubwa wa Boeing 737 kutua katika uwanja huo.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
PROF. Mbarawa Akagua Kivuko Cha MV. Malagarasi, TTCL, POSTA Na Kiwanja Cha Ndege Mkoani Kigoma.
Muonekano
wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala mkoani
Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari sita na
tani 50 kwa wakati mmoja.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto), akipata maelezo Ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa
Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis Choma na Wa
pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka
katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna
ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto)
akijadiliana jambo na Mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV. Malagarasi.
Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS, mkoani kigoma Eng. Narcis Choma
(wa tatu kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), barabara ya Simbo-Kalya yenye
urefu wa zaidi ya Km 200 Kusini mwa Ziwa Tanganyika itakayoanza kujengwa
hivi karibuni wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Uteuzi Wa Bodi Ya Chuo Cha Usimamizi Wa Wanyamapori
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo
cha Usimamizi wa Wanyamapori – Mweka na Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi
ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)
Katika uteuzi huo, Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Profesa Faustin K. Bee kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA. na
Profesa Apolinaria E. Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
Uteuzi huo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 14/3/2016.
Kufuatia uteuzi huo uliofanywa na
Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya
Sheria ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Sura ya 209 kifungu cha 4(3)
kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya 2(1b) amewateua wafuatao kuwa
Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori MWEKA kwa kipindi
cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016.
Wajumbe walioteuliwa ni;
- Samwel Maganga, Professor of Wildlife Management Sokoine University of Agriculture, Morogoro.
- Amani Ngusaru, Country Director, Tanzania World Wildlife Fund for Nature (WWF), Dar es Salaam.
- Andrew Gguga Seguya, Executive Director/CEO of Uganda Wildlife Authority, Kampala.
- Jafari Kidegesho, Department of Wildlife University of Agriculture Morogoro.
- Zuher H. Fazal, Vice Chairman Tanzania Tourism Organization, TATO, Arusha.
- Alexander N. Songorwa, Mkuu wa Chuo cha Mweka, Moshi
- Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania – TAWIRI, Arusha,
- Hassan Mshinda, Director General COSTECH, Dar es Salaam.
- Fred Manongi, Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. – NCAA,
- Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Tanzania -TANAPA, Arusha.
- Herman W. Keraryo, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha kwa mamlaka aliyonayo chini
ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI Sura ya
260 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 aya ya 1(c), Mhe.
Waziri wa Maliasili na Utalii amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi wa taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI kwa
kipindi cha miaka 3 kuanzia tarehe 14/3/2016:
Wajumbe wa walioteuliwa ni;
- Ndelilio A. Urio, Profesa wa Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji Chuo cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
- Martin Loibooki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA.
- Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu, Hifadhi za Taifa TANAPA, Arusha.
- Freddy Manongi, Mhifadhi Mkuu, Mamlaka ya Hifadhi ya. Ngorongoro – NCAA
- Simon Mduma, Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania TAWIRI, Arusha.
- Theresia Nkya, Principal Medical Research Scientist NIMRI, Tanga.
- Revocatus Kurwijila, Professor of Food Science, Chuo cha Kilimo Sokoine Morogoro.
- Hassan Mshinda, Mkurugenzi Mkuu, COSTECH, Dar es Salaam.
- Masound H. Mruke, Profesa, Idara ya Entomolojia na Nyuki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Geophrey Kirenga, Katibu Mtendaji, Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania SAGCOT, Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
No comments:
Post a Comment