Msanii wa Muziki wa Hip Hop, Bongo Kheri Sameer ‘Mr Blue’ Ameendelea
kumporomoshea lawama Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), ambaye pia Ni msanii wa Muziki wa Hip Hop,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa Usumbufu aliokuwa anampa ili kuiachia ngoma
yake ya Freedom Ulimsababishia ‘rabsha’ ndani ya ndoa yake.
Shutuma hizo anazozitoa Blue ni Mwendelezo wa ‘drama’ inayoendelea
kati yake na Sugu ambayo kwa sasa ndiyo Habari ya Mjini kufuatia Madai
ya Blue kuwa Mheshimiwa huyo alimzunguka kwa kuuchukua Wimbo wake huo
ambao mwanzo yeye alimshirikisha, Akaurekodi Upya huku akifuta Mashairi
yake lakini kama haitoshi ‘Akashuti’ video, Jambo ambalo Blue Analiona
kuwa ni Uonevu.
“Kwanza Sugu alinisababishia Matatizo ndani ya Ndoa Yangu mpaka Nikawa sipokei simu zake. Alikuwa ananipigia Simu kila Muda
na kila Siku akiuliza ‘project’ inatoka lini hadi mke wangu akawa
anauliza kuna nini kati yetu.
Mwanzoni nilimweleza hali Halisi lakini
kwa namna Sugu alivyokuwa Ananisumbua ilifika hatua mke wangu akadhani
kuna Jambo lingine Tofauti, kukawepo na rabsha za hapa na pale lakini Sasa Nimeweka Mambo sawa,” alisema Blue.
Alipotafutwa Sugu kuhusu suala hilo, Hakupokea Simu na hata Alipotumiwa Ujumbe mfupi, hakujibu lolote.
No comments:
Post a Comment