Saturday, 30 April 2016

Tanesco Wamezindua Huduma Mpya Kwa Wateja Unaoitwa Tanesco Huduma

Na Mwamvita Mtanda
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limezindua Huduma mpya inayotoa nafasi kwa wateja kutoa na kupata Taarifa kupitia Mfumo wa Mawasiliano uliounganishwa kwenye Simu za kiganjani unaoanza kwa Majaribio katika Mkoa wa kihuduma wa Kinondoni Kaskazini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema jana Jijini Dar es salaam kuwa, mfumo huo ambao uko kwenye programu Maalumu, Utasaidia kuboresha Utendaji Kazi wa Shirika.

“Mfumo huu Utaongeza kasi ya Uwajibikaji wa watendaji kuwahudumia Wananchi, lakini kwa sasa Tumeuanza kwa Majaribio katika Mkoa wetu wa Kinondoni Kaskazini, Wateja wetu watatoa Taarifa za Matukio yanayowakabili hata wale Wanaoomba Rushwa, watujulishe tupate Ushahidi Tuchukue hatua,” alisema Mramba.

Alisema mfumo huo Umeundwa kutokana na Ushirikiano kati ya Tanesco na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech) na alisema itawapunguzia Usumbufu wateja wa kupiga Simu kwenye vituo vya Huduma Wanapokuwa na Malalamiko Binafsi au ya maeneo Wanayoishi.

“Naamini majaribio haya yatakuwa na Mafanikio, Yatawawezesha Wateja wa Tanesco wote nchini kuunganishwa kupata huduma hiyo,” alisema Mramba.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema Hatua hiyo imewapa Moyo wa kuendelea kujituma zaidi kwa kuwa vijana wao Wamepata nafasi ya kuonyesha kiwango cha ubunifu kwenye Masuala ya Teknolojia kulingana na Dunia inavyokwenda.

Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa Tanesco Kinondoni, Nicholaus Kamoleka alisema Mfumo huo unaitwa ‘Tanesco  Huduma’ wateja wataipata kwa kuiomba kupitia Soko la programu la Google liitwilo ‘Play Store’.   


No comments:

Post a Comment