Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Wamempongeza Rais Dkt John Magufuli Ujenzi wa Bomba la Mafuta
Na Mwamvita Mtanda
Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania
(TATOA) pia kimeipongeza timu ya mazungumzo iliyoongozwa na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, huku kikiwataka Wanachama
wake na wadau wote kwa ujumla kuchangamkia fursa nyingi na kubwa za Kibiashara zitakazotokana na Ujenzi wa Bomba hilo.
“Tunatoa shukrani zetu za Dhati kwa
rais wetu na timu iliyoshiriki kwenye Mazungumzo, Wametufanyia Jambo
kubwa katika Ujenzi wa uchumi wa nchi…imebaki Juu yetu kupanga Mikakati
ya namna ya kutumia fursa za kibiashara zitakazoletwa na Mradi huu,”
alisema Mwenyekiti wa Tatoa, Angelina Ngalula jijini Dar es Salaam
Ngalula alisema kutokana na fursa hii
kubwa iliyopatikana, Wadau wote wa Bandari wana Wajibu wa kuitumia
katika kutangaza Bandari Zilizopo nchini ili kuvutia wawekezaji na Wateja katika kukuza Uchumi wa nchi.
“Fursa hii kubwa itaifanya Bandari ya
Tanga kuingia katika Ramani ya Dunia hivyo basi ni Vyema Wadau wote wa Bandari na Wapenda maendeleo kuitumia Vizuri Nafasi hii,” alisema Mwenyekiti na kuongeza kuwa Utekelezaji wa Mradi huo wa Bomba lenye
urefu wa kilometa 1,403 kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga Utatengeneza fursa nyingi za Usafirishaji Mizigo kwa njia ya Reli na Barabara.
No comments:
Post a Comment