Monday, 25 April 2016
Huyu ndo Mtangazaji Anayemkausha Koo Gardner G Habash
Na Kalonga Kasati
Historia ya Emmanuel Kapanga ilianza kuonekana Toka akiwa Kijana Mdogo huko kwako Morogoro Alizaliwa mwaka 25 -12-1988 katka Familia ya Mzee kapanga Toka akiwa Mtoto Mdogo alipenda Sana Kazi ya Utangazaji Mara Zote akiwa na Wenzake alionekana akiwauliza Wenzake Maswali Kama Wanavyofanya Watangazaji Wengine.
Alipohitimu Masomo yake ya Sekondari aliwaambia Wazazi wake anataka kwenda chuo kusomea Uandishi wa Habari Wazazi wake Walimkubaliana nae mwaka 2009 alijiunga na Chuo cha Uandishi Wa Habari Dar es salaam school of Journalism (DSJ)
Akiwa chuo hapo kapanga alikuwa anamudu Vizuri Somo la Radio Broadcasting Ukilinganisha na Masomo Mengine, Mara Zote alikuwa yupo karibu Sana Mwalimu wa Somo Hilo Yusto Santipa kwa kuuliza Maswali ambapo anaona hakuelewa Vizuri katika Mada iliyofundishwa.
Baada ya kumaliza chuo Kapanga alibahatika kupata kazi katika Radio Pambazuka Fm Ambayo ipo Morogoro kama Mtangazaji wa Vipindi vya Burudani na Serious Program Emmanuel alijituma kwa kufanya kazi kwa Bidii ili aweze kutimiza Malengo yake.
Alifanikiwa kuja Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta kazi katika vituo vya Hapa Mjini Akiamini Malengo yangu Yatatimia nikiwa Dar es salaam
Alifanikiwa kupata Kazi Kituo cha EFM ambacho kinafanya Vizuri sana Tishio katika Jiji la Dar es Salaam alianza kama Muandaji wa kipindi cha Ubaoni Mtangazaji akiwa Gardner G Habash na Akifanya Vichekesho kama Mjomba Mjomba chogu mi Siwezi ile ni Sauti yake Emmanuel Kapanga
Baada ya kuondoka Gardner G Habash Uongozi wa EFM Ukaamua kumpa kipindi cha Ubaoni Akisaidiana na Mpoki Seth Maarufu kama Bikra wa kisukuma ambacho kinaanza saa Kumi 10 Jioni Mpaka Saa moja jioni
Kapanga ameendelea kufanya Vizuri katika kipindi cha Ubaoni kwa Jinsi Sauti yake ilivyokuwa Nzuri Na toka Gardner ameondoka Wengi Walidhani kipindi kingekufa lakini kimekuwa Tishio kubwa Sana katika Vipindi vya Jioni kwa kujizolea Wasilizaji Wengi Sana na Mpaka Sasa ndo kipindi Bora
Watangazaji Wengine waige mfano wa Emmanuel Kapanga kwa Nidhamu aliyonayo akiwa Anafanya kipindi amekuwa ni mtu wa kujishusha Sana ananyekea kwa kila mtu ndo maana Hata Mkurugenzi Efm Dj Ma Jay Hajataka kumleta mtu Mwingine katika Kipindi cha Ubaoni Ingawa Uwezo kufanya hivyo anao Ma Jay kwa Gharama Yoyote ile ila ameona Kijana Anamudu Kufanya kipindi cha Ubaoni
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment